Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya viziwaziwa ikiwa ni ziara take ya kikazi ya kusikiliza changamoto na kero.
…………………………………………………………………
NA Victor Masangu,Kibaha
MBunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ameahidi kulivalia njuga suala la changamoto ya afya kwa wananchi wa kata ya viziwaziwa kwa kuweka mipango ya kuanzisha mradi wa kituo Cha afya.
Koka ameyasema hayo wakati wa ziara take ya kikazi kwa wananchi wa kata ya Sagare katika mkutano wa hadhara kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili katika sekta mbali mbali.
Aidha MBunge hiyo aliongeza kuwa anatambua kuwa katika kata ya viziwaziwa Kuna zahanati hivyo katika kuongeza huduma ya afya kwa wananchi ili kuondokana na adha ya kufuata huduma ya matibabu katika maeneo ya mbali.
“Kwa Sasa natambua Kuna zahanati moja katika kata hii ya viziwaziwa lakini kitu kikubwa ni kuipandisha adhi hii zahanati yetu ili iweze kuwa kituo Cha afya na Nina Imani itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kero,”akisema Koka.
Pia Koka alisema katika kuwaboreshea huduma ya matibabu hususan kwa wakinamama wajawazito kwa kuanzisha mradi wa ujenzi wa wodi kwa ajili ya kujifungulia.
Katika hatua nyingine Koka amechangia kiasi Cha shilingi milioni Mbili kwa ajili ya kuanza ujenzi wa shule ya msingi ili kuweza kuwasaidia wanafunzi kutotembea umbari mrefu.
“Kutokana na umuhimu wa elimu na watoto wetu kutembea umbari mrefu mm nachangia kiasi Cha shilingi milioni Mbili ambazo zitaweza kusaidia katika ujenzi huo wa mradi wa shule ya msingi,”alisema Koka.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya viziwa ziwa Mudy Mussa alitoa pongezi kwa MBunge huyo kwa kufanya ziara ya kwenda kusikiliza kero za wananchi licha ya kukabiliaa na baadhi ya changamoto.
Diwani huyo alisema kwa Sasa wanakabiliwa na changamoto ya huduma ya nishati ya umeme.afya pamoja na shule hivyo kunahitajika nguvu za makusudi ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.