Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Hassan Chande akizungumza katika Warsha kwa Wamiliki wa kumbi za starehe na burudani pamoja na viongozi wa dini iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Tifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka akiwa katika Warsha kwa Wamiliki wa kumbi za starehe na burudani pamoja na viongozi wa dini iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NEMC Mhandisi Prof. Esnat Chagu akiwa katika Warsha kwa Wamiliki wa kumbi za starehe na burudani pamoja na viongozi wa dini iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi msaidizi idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Kemilembe Mutasa akiwa katika Warsha kwa Wamiliki wa kumbi za starehe na burudani pamoja na viongozi wa dini iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Wadau mblimbali wa Mazingira wakifuatilia Warsha kwa Wamiliki wa kumbi za starehe na burudani pamoja na viongozi wa dini iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Hassan Chande akipata picha ya pamoja na wamiliki kumbi za starehe na viongozi wa dini katika Warsha kwa Wamiliki wa kumbi za starehe na burudani pamoja na viongozi wa dini iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
******************************
NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM
Jumla ya malalamiko Zaidi ya 85 yameripotiwa kutoka kwa wananchi mbalimbali juu ya matukio yanayohusiana na kelele na mitetemo katika Mkoa wa Dar es Salaam na kwa upande wa Arusha pia kuna idadi kubwa ya malalamiko.
Maeneo yaliyoongoza kwa kulalamikiwa ni kumbi za starehe na burudani kwa kuwa na idadi ya malalamiko 65.
Ameyasema hayo leo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Hassan Chande katika Warsha kwa Wamiliki wa kumbi za starehe na burudani pamoja na viongozi wa dini iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa katika tafiti zilizofanywa, maeneo yaliyo ongoza kwa kusababisha kelele chafuzi ni maeneo ya starehe kwa 33% na viwanda 24%.
Aidha amesema katika kukabiliana na changamoto hizo ni muhimu kuimarisha jitihada za pamoja na ushirikiano miongoni mwa Taasisi za Serikali na wadau ili kusimamia viwango vya Kelele na Mitetemo vilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria.
“Serikali imeanza kuchukua jitihada mabalimbali za kusimamia jambo hili ipasavyo, matharani tayari Ofisi ya Makamu wa Rais na NEMC wamekuta na Wizara mbalimbali katika kulitafutia ufumbuzi jambo hili na kwa Pamoja kama serikali tumekubaliana kelele na mitetemo ni janga linalokuja kwa kasi katika jamii yetu. Pamoja na kuwepo Sheria mbalimbali za kisekta, pia tumeandaa Mwongozo wa udhibiti wa uchafuzi wa Mazingira utokanao na Kelele na Mitetemo ambao unaonesha muundo wa wadau wa utekelezaji wa udhibiti kelele na mitetemo”. Amesema Mhe.Chande.
Naibu Waziri Chande amesema kabla ya uwekezaji wowote haujaanza lazima kufanyike tathimini ya athari kwa Mazingira(EIA) ambayo itasaidia kubainisha changamoto za mradi na sulululisho lake.
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Muhandisi Samuel Gwamaka, akiongea katika Warsha hiyo amesema kuwa kwa kipindi cha hivi karibuni Baraza limepokea taarifa nyingi za malalamiko kutoka kwa wananchi mbalimbali juu ya matukio yanayohusiana na kelele na mitetemo. Hivyo basi ndiyo maana Baraza limeamua kuandaa warsha hiyo kwa Wadau hao kuhusiana na kelele na mitetemo.
”Katika kulitafutia ufumbuzi jambo hili kwa kushirikiana na Wizara mbalimbali, kwa pamoja kama serikali tumekubaliana kelele na mitetemo ni janga linalokuja kwa kasi katika jamii yetu. Pamoja na kuwepo Sheria mbalimbali za kisekta, pia tumeandaa Mwongozo wa udhibiti wa uchafuzi wa Mazingira utokanao na Kelele na Mitetemo ambao unaonesha muundo wa wadau wa utekelezaji wa udhibiti kelele na mitetemo”. Alimalizia Dkt Gwamaka.