WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Villarreal katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
Wageni walitangulia kwa bao la Paco Alcácer dakika ya 53, kabla ya wenyeji kuzinduka kwa mabao ya Alex Telles dakika ya 60 na Cristiano Ronaldo dakika ya 90 na ushei.
Ushindi huo unawafanya Mashetani Wekundu waokote pointi tatu za kwanza kwenye kundi hilo kufuatia kuchapwa 1-0 na Young Boys kwenye mchezo wa kwanza Uswisi.