MKurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Michezo Bw.Nsolo Mlozi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo September 30,2021 wakati akitangaza Mbio za Capital City Marathon Dodoma zitakazofanyika October 10 mwaka huu jijini Dodoma na Mgeni rasmi anatarajia kuwa Naibu Spika Dkt.Tulia Ackson.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja Shirika la Bima la Taifa (NIC),Yessaya Mwakifulefule, akielezea jinsi walivyoamua kudhamini Mbio za Capital City Marathon Dodoma zitakazofanyika October 10 mwaka huu jijini Dodoma na Mgeni rasmi anatarajia kuwa Naibu Spika Dkt.Tulia Ackson.
Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dodoma,Robert Mabonye,akiwapongeza waandaaji wa Mbio za Capital City Marathon Dodoma kwa kuamua kuzifanyia Jijini hapa ambazo zinatarajia kufanyika October 10 mwaka huu jijini Dodoma na Mgeni rasmi anatarajia kuwa Naibu Spika Dkt.Tulia Ackson.
Wakionyesha Medali zitakazotumika kuwapa washindi katika Mbio za Capital City Marathon Dodoma.
Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja Shirika la Bima la Taifa (NIC),Yessaya Mwakifulefule,ambao ndio wadhamini wakuu Mbio za Capital City Marathon Dodoma akionyesha Jezi itakayotumika katika Mbio hizo zitakazofanyika October 10 mwaka huu jijini Dodoma na Mgeni rasmi anatarajia kuwa Naibu Spika Dkt.Tulia Ackson.
MKurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Michezo Bw.Nsolo Mlozi,akisisitiza watu kushiriki Mbio za Capital City Marathon Dodoma zitakazofanyika October 10 mwaka huu jijini Dodoma na Mgeni rasmi anatarajia kuwa Naibu Spika Dkt.Tulia Ackson.
Wadhamini wa Mbio za Capital City Marathon Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangaza Mbio hizo ambazo zitakazofanyika October 10 mwaka huu jijini Dodoma na Mgeni rasmi anatarajia kuwa Naibu Spika Dkt.Tulia Ackson.
Wandaaji wa Mbio za Capital City Marathon Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangaza Mbio hizo ambazo zitakazofanyika October 10 mwaka huu jijini Dodoma na Mgeni rasmi anatarajia kuwa Naibu Spika Dkt.Tulia Ackson.
……………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Michezo, Bw. Nsolo Mlozi ,amezindua rasmi mashindano ya Mbio za Capital City Marathon Dodoma zinazotarajia kufanyika ya octoba 10,2021 katika barabara za Chou kikuu cha Dodoma (UDOM) zitakazowashirikisha watu Wazima pamoja na Watoto.
Hayo ameyasema leo September 30,2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari Mlozi,amesema kuwa Mgeni rasmi anatarajia kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Akson
Amesema kuwa mbio hizo zitashirikisha washiriki zaidi ya 2000 ambao watashirika katika mbio za kilometa 21.1 kwa Watu 700,kilometa 10 kwa watu 800 na kilometa 5 kwa watu 500 na gharama kila Mshiriki ni Elfu 40,000
”Leo rasmi tunatangaza tarehe 10/10/2021 tutafanya mbio yetu ya pili kubwa ambayo inaitwa Second City Marathon ambayo itafanyika katika chuo kikuu cha Dodoma” amesema Mlozi
”Jiji la Dodoma limepata wageni wengi waliohamia ,muda unapatikana mwingi sana jioni tunapotoka ofisini,kwahiyo tumeona tuboreshe urafiki wetu na undugu wetu katika michezo ,sambamba na hayo tumekuwa tukifanya shughuli mbalimbali ikiwemo mbio za michezo kwa kila mwezi’
Aidha amesema kuwa Mbio hizo zinashirikisha watu kutoka nje na ndani ya Tanzania lengo la kufanya hivi itasaidia kukuza utali wa Dodoma na wameandaliwa mazingira mazuri ya kushiriki na hatukauwa na usumbufu na lila mmoja atapata vifaa kila eneo alilopo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa wateja la Bima ya Taifa (NHC) ,Yessaya Mwakifulefule ,amesema wana furaha ya kushirikiana na Capital City Marathon kwa kudhamini mbio hizo .
‘’Sisi kama NIC tunaamini kuwa marathon hizi ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi ,tunaona ndugu zetu wakenya wanafanya vizuri katika eneo hilo lakini kabla ya hapo tulikuwa tukitamba miaka ya nyuma Tanzania halafu kidogo vijapi vikapotea ”amesema
Aidha amesema kuwa wanaahidi kuwa wataendelea kudhamini mbio hizo na kutoa zawadi kwa washiriki ili kuhamasisha watu pamoja kuunga mkono michezo Tanzania na kuwaomba watanzania kutumia BIMA
Naye Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dodoma,Robert Mabonye, amewasisitiza wakazi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kuhudhuria katika mbio hizo
‘’ Niwaambie wakazi wa Dodoma hii ni fursa wajitokeze kwa wingi sisi Dodoma tuwe wa kwanza kuchukua donge nono iliyotolewa na Capital City Marathon’’amesema