Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati akizindua Mwongozo wa sera ya nyongeza ya ushirikiano wa majukumu baina ya kada za afya kuhusu ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto na ujazaji wa fomu za PF3 hafla iliyofanyik leo September 29,2021 jijini Dodoma.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi.Agnes Mtawa,akielezea mkakati wa Mwongozo wa sera ya nyongeza ya ushirikiano wa majukumu baina ya kada za afya kuhusu ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto na ujazaji wa fomu za PF3 hafla iliyofanyik leo September 29,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIP Bi.Saida Mukhi,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa sera ya nyongeza ya ushirikiano wa majukumu baina ya kada za afya kuhusu ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto na ujazaji wa fomu za PF3 hafla iliyofanyik leo September 29,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa TIP Sheikh Mfaume,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa sera ya nyongeza ya ushirikiano wa majukumu baina ya kada za afya kuhusu ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto na ujazaji wa fomu za PF3 hafla iliyofanyik leo September 29,2021 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya Bw.Samwel Koyo, akizungumzia malengo ya Mkutano huo wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa sera ya nyongeza ya ushirikiano wa majukumu baina ya kada za afya kuhusu ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto na ujazaji wa fomu za PF3 hafla iliyofanyik leo September 29,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wakifatilia hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,(hayupo pichani) wakati akizindua Mwongozo wa sera ya nyongeza ya ushirikiano wa majukumu baina ya kada za afya kuhusu ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto na ujazaji wa fomu za PF3 hafla iliyofanyik leo September 29,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akizindua Mwongozo wa sera ya nyongeza ya ushirikiano wa majukumu baina ya kada za afya kuhusu ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto na ujazaji wa fomu za PF3 hafla iliyofanyik leo September 29,2021 jijini Dodoma.
Dodoma Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akionyesha Mwongozo wa sera ya nyongeza ya ushirikiano wa majukumu baina ya kada za afya kuhusu ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto na ujazaji wa fomu za PF3 hafla iliyofanyik leo September 29,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya Bw.Samwel Koyo Mwongozo wa sera ya nyongeza ya ushirikiano wa majukumu baina ya kada za afya kuhusu ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto na ujazaji wa fomu za PF3 hafla iliyofanyik leo September 29,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akimkabidhi Mwenyekiti wa TIP Sheikh Mfaume, Mwongozo wa sera ya nyongeza ya ushirikiano wa majukumu baina ya kada za afya kuhusu ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto na ujazaji wa fomu za PF3 hafla iliyofanyik leo September 29,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akimkabidhi Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi.Agnes Mtawa,Mwongozo wa sera ya nyongeza ya ushirikiano wa majukumu baina ya kada za afya kuhusu ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto na ujazaji wa fomu za PF3 hafla iliyofanyik leo September 29,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Mwongozo wa sera ya nyongeza ya ushirikiano wa majukumu baina ya kada za afya kuhusu ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto na ujazaji wa fomu za PF3 hafla iliyofanyik leo September 29,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt Doroth Gwajima amezinduzi Mwongozo wa sera ya nyongeza ya ushirikiano wa majukumu baina ya kada za afya kuhusu ukatili wa kijinsia, ukatili dhidi ya watoto na ujazaji wa fomu za PF3.
Pia amesema kuwa Mwogozo huo utawezesha wahanga wa ukatili wa kijinsia wanawake na watoto kupata huduma bora za matibabu.
Akizundua leo Septemba 29,2021,Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi huo ambao ulihudhuriwa na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Dini,Waziri Gwajima amesema mwongozo huo utasaidia kupambana na changamoto ya ukatili wa kijinsia katika jamii.
Waziri Gwajima amesema uwepo wa sera hiyo kutawezesha wahanga wa ukataili wa kijinsia na watoto kupata huduma bora za matibabu kutokana na kuboreshwa kwa mfumo wa ujazaji wa fomu za PF3.
“Sera hii itawezesha pia kupatikana kwa urahisi ushahidi wa mtu aliyefanyiwa ukatili wa kijinsia hivyo kuondoa changamoto iliyopo hivi sasa ya kesi nyingi za ukatili wa kijinsia kukosa ushahidi wa kutosha”amesema Dk.Gwajima
Aidha Waziri Gwajima ametoa wito kwa watumishi wa kada ya afya kuusoma ili wauelewe mwongozo huo ambapo amedai suala la ukatili wa kijinsia bado ni tatizo katika jamii hivyo zinahitajika juhudi za pamoja kutokemeza jambo hilo.
Waziri Gwajima amesema mila na desturi potofu bado zipo katika jamii hivyo kila mmoja anatakiwa kupambana kuhakikisha tatizo hilo linaondoka.
”Ili kukabiliana na jambo hilo zinahitajika mbinu za ushirikiano katika makundi yote,kuondoa aina zote za ukatili wa kijinsia,kuzuia aina mpya na ya zamani kujitokeza pamoja na elimu endelevu kwa jamii”aamesisitiza
Waziri Gwajima amesema kuwa Mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000), Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Jinsia (2005), Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008), Sheria ya Makosa ya Kujamiiana – SOSPA (1998).
Pia amesema kuwa bado wanakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa ushahidi pindi watuhumiwa wanapopelekwa katika vyombo vya sheria.
“Pamoja na uwepo wa mpango hatuwezi kufikia malengo haya kama hatutawajibika kwa pamoja katika kupiga vita suala la ukatili wa kijinsia, hivyo tunahitaji kuwa na mbinu mbalimbali zinazoweza kutumika kufanikisha malengo haya.”amesema
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Tanzania Interfaith Patnership (TIP) Sheikhe Khalid Mfaume amesema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinakadiria takribani wasichana milioni 150 na wavulana milioni 73 chini ya miaka 18 wameishafanyiwa vitendo mbalimbali vya ukatili na udhalilishaji.
Amesema jambo hilo ni changamoto ambayo sio ya kufumbiwa macho kwani maendeleo endelevu hupatikana kwa kuweka mazingira mazuri kwa watoto.
”Katika kipindi cha miaka mitano wamejikita katika mambo yanayohusu ushawishi wa kusimamia mambo ya watoto malezi na usafi ambapo mwaka huu wanatarajia kutanua zaidi huduma kufikia ulinzi wa mtoto na kusimamia masuala ya lishe kwa mtoto”amesema
Awali Kaimu mkurugenzi wa huduma za uuguzi na ukunga wizra ya afya Sanwel Koyo, amesema kuwa sera hiyo inalenga pia kuwa na jamii yenye afya njema ili kujenga uchumi imara wa Taifa.
Naye Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)Jabir Mruma amesema wameendelea kutoa elimu kwa waumini wa dini ya kiislamu kuhusiana na umuhimu wa chanjo ya ugonjwa wa Uvico 19.
“Tumeendelea kutoa elimu juu ya chanjo ya ugonjwa wa Uvico 19 na sisi tumechanja na tupo vizuri ,sisi viongozi wa dini tutaendelea kushirikiana na Serikali yetu katika mambo mbalimbali,”amesema