Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa (MSD), Meja Jenerali Gabriel Mhidze akizungumza na waandishi wa habari kwenye semina ya siku moja iliyoandaliwa na MSD iliyokuwa na lengo la kutoa taarifa ya mafanikio na mwelekeo wa MSD, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD Erick Mapunda.
Wafanyakazi wa MSD wakiwa kwenye semina hiyo.
Waandishi wa Habari wakiwa kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.
***********************************
Na Dotto Mwaibale
MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Meja Jenerali Gabriel(Dkt) Mhidze amesema MSD iko mbioni kuanzisha kiwanda cha dawa za ngozi,ikiwemo mafuta maalumu ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Meja Jenerali Mhidze aliyaeleza hayo jana mbele ya waandishi wa habari alipokuwa akizungumzia kuhusu majukumu na maboresho ya MSD.
Alisema kiwanda hicho, ambacho mashine zake zimeshafika kitazalisha pia dawa za meno na dawa za macho.
Aidha Mkurugenzi Mkuu huyo wa MSD ameeleza kuwa kiwanda cha MSD cha kuzalisha mipira ya mikono kilichopo imIdofi, Makambako mkoani Njombe kinatarajiwa kuanza uzalishaji mwezi Novemba mwishoni,huku akisema viwanda vingine vya dawa za rangi mbili, vidonge na dawa za maji maji za watoto mashine zake zimeshaanza kuwasili.
Tayari ina viwanda vya kuzalisha barakoa na dawa Keko jijini Dar es Salaam,ambavyo vinauwezo wa kuzalisha aina 10 za dawa na barakoa.