Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu,akizungumza wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) hafla iliyofanyika leo September 28,2021 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Prof Riziki Shemdoe,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) hafla iliyofanyika leo September 28,2021 jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) hafla iliyofanyika leo September 28,2021 jijini Dodoma.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa TARURA wakifuatilia hotuba za Viongozi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Baraza hilo hafla iliyofanyika leo September 28,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu,akizundua Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) hafla iliyofanyika leo September 28,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu (Mb), akifurahia jambo baada ya uzinduzi wa Barza la Wafanyakazi wa TARURA katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor H. Seff na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TARURA Bi. Julieth Magambo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) hafla iliyofanyika leo September 28,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
SERIKALI imeutaka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kutimiza azma ya Rais Samia kwa kusimamia ujenzi wa barabara kwa ubora kufuatia ongezeko la bajeti kwa mwaka 2021/22.
Kauli hiyo imetolewa leo September 28,2021 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA).
Amesema matamanio ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona miundombinu ya barabara inaboreshwa ndio maana ameongeza bajeti kutoka Sh bilioni 277 mpaka Sh bilioni 966 kwa mwaka wa fedha 2021/22.
“ Ongezeko la bajeti ni kubwa inatakiwa kazi itakayofanyika ionekane na iwe na ubora na tuweze kuacha alama na kumbukumbu kwa kazi kubwa aliyoifanya Mhe. Samia Suluhu kupitia Serikali ya Awamu ya Sita,” amesema Ummy.
Aidha amefafanua kuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hasan wakati akufungua Mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa alisisitiza kwenye thamani ya fedha za miradi inayotekelezwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na akatuagiza kuhakikisha thamani ya fedha ionekane kwenye miradi yote tunayoitekeleza nasisitiza kwenu ubora wa Barabara zinazoenda kujengwa ukaonekane.
“Katika mpango mkakati wenu mliojiwekea wa Miaka mitano mmeweka kujenga Barabara za Lami zenye urefu wa Km 1455 nikizigawanya kwa mwaka ni kama Km 291 nataka kuziona barabara zikijengwa kwa ubora wa hali ya juu” amesema
Pia Waziri Ummy amesema kuwa kwenye barabara za udongo mtandao wa barabara uliopo hivi sasa ni km 29,000 lakin mpango wa miaka mitano ni kujenga barabara za changarawe zenye urefu wa kilometa 100,200 niwatake mzingatie ubora wa katika ujenzi wa barabara hizi.
Hata hivyo ameitaka TARURA kuweka kipengele cha tafiti katika bajeti zao ili kuweza kupata teknolojia nzuri itakayotusaidia kujenga barabara zenye ubora na zitakazodumu kwa muda mrefu kwa gharama nafuu.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff , amesema lengo la kuanzisha baraza ni kulinda masilahi ya wafanyakazi kwa kuwa wao ndio wanafanyia kazi na kuwasirisha malalamiko yao.
Aidha amesema anafurahishwa na wadau wanaondelea kuwaunga mkono na kuangalia jitihada zao ambazo zinawajengea uaminifu kwa wananchi na wanatarajia mwaka huu kujenga kilometa 234 za barabara ya lami na za changalawe Zaidi ya elfu 11,000 na madaraja zaidi ya elf 2000.
“Kama wafanyakzi watakuwa na malalamiko hii ndio itakuwa sehemu yao ya kuwasilisha ambapo itajadiliwa nakupatiwa ufumbuzi pia hii itasahidia kuangalia utendaji wa TARURA