MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Simba SC imeshindwa kutamba ugenini baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
Simba wakiamini kuwa wanaondoka na Pointi 3 muhimu mara baada ya kupata Penalti ambayo ilipigwa na Mshambuliaji wao hatari John Bocco na kupanguliwa na kipa Mganda, Cleo James Ssetuba dakika ya 90.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, bao pekee la Cleophace Mkandala dakika ya 33 limewapa wenyeji, Dodoma Jiji FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Na Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, bao la Peter Mapunda dakika ya 90 na ushei limeipa Mbeya City ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.