Home Mchanganyiko RAIS SAMIA AITAKA ALAT KUSIMAMIA KIKAMILIFU 10% INAYOTOLEWA NA HALMASHAURI NCHINI

RAIS SAMIA AITAKA ALAT KUSIMAMIA KIKAMILIFU 10% INAYOTOLEWA NA HALMASHAURI NCHINI

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika leo September 27,201 Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa  Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika leo September 27,2021 jijini Dodoma

   

Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika leo September 27,201 Jijini Dodoma

………………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,ameitaka Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) kuhakikisha inasimamia kikamilifu 10% inayotolewa na Halmashauri nchini.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo September 27,2021 jijini Dodoma wakati  akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT)

Rais Samia amesema kuwa Halmashauri zianze kutoa fedha hizo kwa vikundi vikubwa kwenye miradi mikubwa ambayo manufaa yake yataonekana kuliko kutoa fedha kidogo kidogo kwasababu itaua mfuko huo kwa maslahi binafsi.

”Bado kuna shida kwenye thamani ya fedha kwa miradi mnayoitekeleza, fedha nyingi zinakuja kwenu lakini miradi haifanani na fedha zinazotolewa, pamoja na kwamba tutaendelea kuleta fedha naagiza thamani ya fedha katika miradi tunayoitekeleza ionekane”amesisitiza Rais Samia

Hata hivyo Rais Samia amesisitiza kusimamia makusanyo na matumizi katika halmashauri zetu, Serikali za Mitaa wamekuwa wamekuwa wakitumia  fedha, ningependa kuona ALAT na uongozi wa TAMISEMI mnayasimamia hayo.

Aidha Rais Samia ameiagiza ALAT kutumia mitandao katika kazi zao kutoa taarifa za Serikali za mitaa kukusanya mapato na kuweka rekodi za huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Tutaendelea kuleta wataalam wa kada mbalimbali na kuwajengea uwezo pia kwa kadri uwezo wa Serikali utakavyokuwa ukiongezeka tutaendelea kuangalia maslahi ya Madiwani na watendaji wengine kwenye Halmashauri zetu .

Aidha amesema kuwa Kuhusu suala la ushirikishwaji wa wananchi kwenye miradi ya maendeleo Rais Samia amesema ni jambo la msingi kwa ajili ya maendeleo huku akiahidi kujenga madarasa 15,000 kote nchini  hivyo mwezi januari hakutakuwa na migawanyo ya awamu kuripoti  shuleni kwa kigezo cha kukosa vyumba vya madarasa.

‘Kipaumbele ca Serikali ya awamu ya sita ni katika masuala ya Elimu,kujenga zahanati pamoja na miundombinu lengo likiwa ni kuboresha huduma zote za kijamii kwa wananchi.”

Hata hivyo ameeleza kuwa suala la  kero mbalimbali kwa wananchi ikiwemo migogoro ya mirathi na migogoro ya ardhi Rais  Samia amewataka viongozi serikali za mitaa kutenda  haki.

 Rais Samia amesema Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI imekuwa ikiongoza kwa kutengewa fedha nyingi ambapo katika bajeti ya mwaka huu wa fedha TAMISEMI imetengewa kiasi cha shilingi Trilioni 7.3 takribani asilimia 20 ya bajeti yote ya serikali.

Kwa upande wake Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa ,amesema kupitia mfumo wa Force Account kumekuwa na uaminifu katika halmashauri kutokana na utekelezaji miradi ya Maendeleo hivyo  naitka ALAT kufanya kazi kwa weledi .

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu, amesema kuwa maamuzi ya serikali kuanza kulipa posho madiwani limepokelewa vyema kwani imerudisha hadhi na heshima kwa Madiwani.

”Nawatka  viongozi wote kusimamia vyema miradi ya maendeleo  ambapo hadi sasa halmashauri zimeshapokea Tsh.bilioni  298 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo”amesema Waziri Ummy

Mkutano  mkuu  maalum wa ALAT unakwenda  sambamba na kauli mbiu isemayo”Chagua viongozi bora  kwa maendeleo endelevu “ambapo  uchaguzi wa ALAT unaongozwa na kanuni za kudumu  ukihusishwa na wajumbe mbalimbali ikiwemo Mayeya wa majiji na manispaa na wakurugenzi wa halmashauri kote nchini.