Mjumbe wa kamati Kuu ya chama cha Act Wazalendo Ismail Jussa Ladhu akimtambulisha kwa wapiga kura mgombea wa Chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kondo katika nafasi Ubunge Muhammed Said Issa katika uzinduzi wa kampeni Uliofanyika Viwanja vya Okapi Msuka Wilaya ya Micheweni Jimbo la Konde
Mjumbe wa kamati Kuu ya chama cha ACT Wazalendo Ismail Jussa Ladhu amewataka wananchi wa jimbo la konde kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 9 October 2021 kwa ajili kupiga kura wakiwa wanajiamini wanayemtaka ataibuka mshindi.
Jussa aliyaeleza hayo huko Msuka katika kiwanja cha okapi, Wilaya ya Micheweni wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la konde.
Aliwaambia wasiwe na woga wowote wajitokeze kwa wingi kumchagua Mgombea wa ACT wazalendo Muhammed Said Issa ili awawakilishe katika Bunge kwa ajili ya kupaza sauti zao.
“ tumchagueni Muhammed ili awe sauti ya watu wa Konde na wazanzibar kwa ujumla akasimamie maslahi yetu, na vizazi vyetu” alieleza Jussa.
Aliseme kuwa wasiwetayari kupokea ulaghai wa CCM wakijidai kuleta maendeleo na kudai hawana wanaloweza kuwaletea ispokuwa vurugu na ahadi zisizotekelezeka.
“Chama pekee kinachoweza kuleta maeendeleo ni ACT wazalendo kwani Viongozi wake wanauthubutu wa kudai chochote chenye Maslahi ya Zanzibar” alisema.
“Tulikuwa tukimsikia Mbunge wetu ambaye ni marehemu alivyokuwa akiitetea Zanzibar Marehemu Khatib Said, kwa hiyo tumchagueni Muhammed ili akaendeleze pale alipopaacha marehemu” aliendelea Jussa.
Aliwataka Vijana wasiwe ni wenye kukata tamaa katika kutafuta mabadiliko ya Zanzibar kutokana na Vitimbi vinavyofanywa na baadhi watu aliowataja kuwa hawatakii mema Zanzibar.
“Vijana tukikata tama tutakuwa Masuuli kwa kazi kubwa ambayo wazee wetu wameifanya kwa maslahi ya nchi yetu” alieleza Jussa ambaye alikuwa Mjumbe wa baraza la wawakilishi kupitia Jimbo la Mji Mkongwe.
Alisema kuwa kwa upande wake hana ghofu na wapiga kura kwani Wapemba hawajawahi kuipigia kura CCM, bali aliitaka tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendesha uchaguzi huo kwa misingi ya haki na huru.
Alisema Uchaguzi uliopita Mgombea aliejiuzu, Tume kwa kushirikiana na kile alichodai watu ambao hawana nia njema na Zanzibar waliweza kuuingilia uchaguzi na kuuvuruga.
“Nna waambia NEC tunaingia kwenye uchaguzi na tutalinda ushindi wetu na hatukotayari kuona tunaonewa” alisema Jussa.
Mapema Kaimu Katibu Mkuu ambaye pia ni Katibu wa habari na uenezi wa chama hicho Salim Biman aliwataka wananchi wa konde waende kwenye Vituo na huku wakijiamini kuwa mgombea wao atashinda na atatangazwa na yeyote atakayehujumu uchaguzi chama kitapambana naye na kuwahakikishia kuwa haki itasimama.
Naye Mgombea wa Jimbo hilo kupitia ACT Wazalendo Muhammed Said Issa alisema yuko tayari kuwa Mbunge wa watu wa konde ili aweze kuwasemea katika Chombo hicho cha kutunga Sheria.
alikishukuru Chama chake kwa kile alichodai kuwa baada ya dhulma kilifanyakazi kubwa na mpaka uchaguzi umerejewea na yeye kurudi tena kuwa mgombea.
“Basi mara hii iwe zaidi na zaidi Tuchague mbunge ambaye tunamuhitaji ambaye ni mimi, kwani hili Jimbo ni la kwetu na nakuombeni tuende mkanichague kwa kura nyingi mnoo” alisema Issa
Alisema kuwa endepo wapiga wa kura wa Jimbo hilo wakampatia kura za kutosha atahakikisha anatatu zile kero ambazo zimewazunguka.
“Marehemu Khatib alifanya mengingi mazuri nipeni kura zenu niendeleze pale alipopaacha” alisema Issa.
Aliwataka wananchi wa Konde kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kumchagua yeye kwa kura nyingi ili aibuke na ushindi wa asilimia 95.
Uchaguzi huo umerejewa baada ya aliyekuwa mshindi wa Uchaguzi Mdogo Sheha Mpemba uliofanyika tarehe 18 Julai mwaka huu kujiuzulu kabla ya kula kiapo Bungeni kwa kile alichodai matatizo ya kifamilia pamoja na vitisho kumuandama. Kauli hiyo ya Sheha ilipata Baraka zoote kutoka kwa chama chake cha CCM, ambapo katibu mwenezi Shaka Hamdu Shaka alikubalia na maamuzi ya Mpemba na badae Tume