Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Wilaya ya Dodoma Mjini waliofika kumpokea katika eneo la Chinangali mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea Jijini Dar essalaam leo tarehe 26 Septemba ,2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akivalishwa Vazi la Kimila na Wazee wa Kimila wa Kabila la Kigogo wenye asili ya Dodoma Wilayani Chamwino kama ishara ya ukaribisho mara baada ya kuwasili Chamwino Ikulu akitokea Jijini Dar es salaam leo Sept 26,2021.
Mzee wa Kimila wa Kabila la Kigogo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma Bw. Goden Wenga akimkabizi Ngao na Mkuki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kama ishara ya ukaribisho mara baada ya kuwasili Chamwino Ikulu akitokea Jijini Dar es salaam leo Sept 26,2021. PICHA NA IKULU.