Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde,akizungumza wakati akifunga Mafunzo ya wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyomalizika leo September 25,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde,wakati akifunga Mafunzo ya wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyomalizika leo September 25,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wametakiwa kusimamia nidhamu ya watumishi waliochini yao ili kuhakikisha wanatenda haki na kufuata miongozo kanuni na sheria za utumishi wa umma
Kauli hiyo imetolewa leo September 25,2021 jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde wakati akifunga Mafunzo ya wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Mhe. Silinde amesema amewataka kuhakikisha wanazingatia mipaka ya madaraka na hatua zinazochukuliwa dhidi ya watumishi zifuate sheria, kanuni na taratibu za utendai kazi katika utumishi wa umma na Serikali kwa ujumla.
Mhe. Silinde amesema ni wajibu wa wakurugenzi kuhakikisha wanatatua kero za wananchi ameaagiza wakurugenzi hao kutatua kero za wananchi hasa walioko maeneo ya vijijini ambao wengi ni masikini kwa kuhakikisha wanapatikana kirahisi maofisini na kuondoa urasimu usio wa lazima.
”Bado kuna maeneo fedha za Serikali zinapotea na kuingia katika mifuko ya wajanja kwa kutumia risiti za mikono, hivyo nawataka mtumie mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato”amesema Mhe.Silinde
Aidha amewagiza kuhakikisha wanasimamia matumizi sahihi za fedha za Serikali na zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na kulingana na thamani ya fedha zilizotumika ikilinganishwa na huduma iliyotolewa.
”Hakikisheni mnasimamia ubunifu na uhodari katika kutekeleza wajibu wenu kwa kuzingatia mipango ya wananchi kupitia Halmashauri zenu na hakikisheni mnasimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri zenu”amesema
Hata hivyo Mhe. Silinde amesema ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi vi vyema wakaongeza kasi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za waalimu , vituo vya afya, vituo vya maji safi na salama.