Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu akiwa sambamba na madiwani wa viti maalum manispaa ya Iringa pamoja na viongozi wa Machinga IringaMadiwani wa viti maalumu(CCM) Iringa wakiwa na viongozi wa Machinga mkoa wa Iringa wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu wakati akiongea na machinga wa Manispaa ya Iringa.Baadhi ya wafanyabishara wadogowadogo waliojitokeza kumsikiliza mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu wakiwa na mabango yaoBaadhi ya wafanyabishara wadogowadogo waliojitokeza kumsikiliza mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wafanyabiashara wadogo wadogo wa
manispaa ya Iringa (machinga) wamesema kuwa hawapo tayari kuondoka katika eneo
la mashine tatu na miomboni kwa kuwa maeneo hayo ndio ambayo yanawateja wengi
wanaonunua bidhaa kwa wingi tofauti na maeneo mengine hapa manispaa.
Wakizungumza kwenye mkutano
waliofanya na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu walisema kuwa
wanaheshimu na kufuata maagizo yote ya Waziri mkuu Pamoja na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya kuwa machinga wapangwe vizuri na sio kuondoshwa kwenye
maeneo yao.
Walisema kuwa eneo la mashine
tatu wamekuwa wakifanyia biashara zao kwa miaka mingi na limezoeleka kwa
wanunuzi wengi kwenda kununua bidhaa ndogo ndogo katika eneo hilo inakuaje sasa
wanataka kuwaondoa katika eneo hilo la kibiashara ambalo wao ndio
wamelitengeneza kwa kiasi kikubwa.
Wachinga hao waliongeza kwa
kusema kuwa hawapo tayari kuondoka na hawezi kuondoka katika eneo hilo ambalo
limekuwa linamzunguko mkubwa wa biashara tofauti na maeneo mengine ambayo
inasemekana serikali ya halmashauri ya manispaa ya Iringa imepanga kuwapeleka
huko.
Aidha machinga machinga hao
walisema kuwa wanaiomba serikali ya manispaa ya Iringa kufuata maagizo ya Waziri
mkuu ambayo aliyatoa kuhusu namna ya mpangilio mzuri wa wafanyabiashara wadogo
wadogo.
Walisema kuwa wamekuwa
wanachangia mapato serikalini bila tatizo lakini na kukuza uchumi wa Manispaa nan
chi kwa ujumla iwaje ghafla wanataka kuwaondoa kwenye maeneo ambavyo wamezoea
kuyafanyia kazi kila siku.
Kwa upande wake katibu wa
Machinga Network mkoa wa Iringa Joseph Kilienyi alisema kuwa serikali ya
halmashauri ya Manispaa ya Iringa alisema kuwa wafanyabiashara hao wapo tayari
kupangwa kwenye maeneo wanayofanyia baishara na sio kuondolewa kwenye maeneo
hayo ambayo wamekuwa wanafanyia baishara kwa miaka mingi bila kusumbuliwa.
Alisema kuwa kuwaondoa machinga
kwenye maeneo ambayo wanayafanyia kazi litakuwa jambo gum una haliwezekani hata
siku moja hiyo ni lazima serikali ijipange kuhakikisha inatatua jambo hilo kwa
kufuata muungozo wa Waziri mkuu.
Kilienyi alisema kuwa anaamini
kwenye majadiliano tofauti na kutumia nguvu kama ambavyo baadhi ya viongozi
kwenye maeneo mengine wamekuwa wakitumia nguvu kuwaondoa machinga kwenye maeneo
ambayo wameyazoea kufanyia kazi biashara zao.
Alisema kuwa wapo tayari kufuata
sheria zote za nchi na kuondoka katika maeneo hatarishi kama kwenye mifereji na
maeneo mengine kama hayo lakini sio maeneo ambayo wanataka kuwapeleka hivi sasa
ambayo kwa kiasi kikubwa sio rafiki na biashara zao.
Kilienyi alisema kuwa
wafanyabiasahara wadogo wadogo wamekuwa wanafanya biashara zao katika maeneo
hayo kama mbadala wa kuajiliwa na serikali kwa kuwa hivi sasa ajira zimekuwa
ngumu kupatika hivyo njia mbadala ni kufanya biashara.
Alisema kuwa kuwaondoa machika
katika maeneo ambayo wamezoea kuyafanyaia kazi ni kupunguza kasi ya kukuza
uchumi wananchi na kufifisha maendeleo ya nchi kwa kuwa machinga wamekuwa
msaada mkubwa kwa serikali kukuza uchumi wan chi na kuongeza thamani ya mitaji
ya matajiri.
Kilienyi alisema kuwa hawapo tayari
kuondolewa katika barabara ya mashine tatu bali wapo tayari kupangwa kwenye mpangilio
mzuri unaostahili hivyo uongozi wa halamshauri ya Manispaa ya Iringa wanapaswa
kufikiri upya kuhusiana na mpango wao.
Naye mbunge wa jimbo la Iringa mjini
Jesca Msambatavangu aliwataka wafanyabiashara waodogo wadogo kuwa na subira
wakati serikali ya halmashauri ya Iringa wakijipanga kuhakikisha wanatatua
mgogoro huo na kuwapanga vizuri kwenye eneo hilo la mashine tatu ambalo
limekuwa na mzunguko mkubwa wa biashara.
Alisema kuwa machinga wanatakiwa
kupangwa kwenye mpangilio mzuri ambao utakuwa rafiki kwao wakati wa kufanya
biashara zao.
Msambatavangu aliwataka wamachi
kuwa wasafiri na kuondoka mara moja kwenye maeneo hatari ambayo yamekuwa
yanaathiri afya zao na mienendo ya biashara zao kwa ujumla.
Alimalizia kwa kusema kuwa
serikali ya halmashauri ya wilaya ya Iringa wapo kwenye mjadala wa namna gani
wafanyabiashara hao watafanya baishara zao bila kusumbuliwa na mtu yeyote yule.