Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Ummy Mwalimu,akizungumza wakati akifungua Mafunzo ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofanyika leo September 24,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Mhe. David Silinde,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofanyika leo September 24,2021 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Prof Riziki Shemdoe,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofanyika leo September 24,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Ummy Mwalimu, wakati akifungua Mafunzo ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofanyika leo September 24,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Shirika la UNCDF Bw.Peter Marika,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofanyika leo September 24,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Ummy Mwalimu,akizindua Mwongozo wa uandaaji wa miradi ya kimkakati inayozalisha mapato kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa mara baada ya kufungua Mafunzo ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofanyika leo September 24,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Ummy Mwalimu,akiwa amenyanyua Vitabu Vikionyesha Mwongozo wa uandaaji wa miradi ya kimkakati inayozalisha mapato kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa mara baada ya kufungua Mafunzo ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofanyika leo September 24,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Ummy Mwalimu,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mafunzo ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofanyika leo September 24,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. @ummymwalimu amesema Wakurugenzi wa Halmashauri kupimwa kwa kigezo cha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo inayotatua kero za wananchi.
Kauli hiyo ameitoa leo September 24,2021 jijini Dodoma wakati akifungua Mafunzo ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Waziri Ummy ameendelea kusema kuwa agenda ya mapato inaenda sambamba na kigezo cha kupima kiasi cha fedha kilichotolewa na Halmashauri katika kutatua kero za wananchi hususani katika miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, barabara, Masoko, na kuwekeza kiuchumi wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Waziri Ummy amewataka kuhakikisha wanatenga asilimia 40 ya mapato ya ndani yasiyolindwa inatengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa Halmashauri ambazo zinapata mapato chini ya Bilioni 5 na wale wanaokusanya zaidi ya bilioni tano wanatakiwa kutenga asilimia 60
Anaendelea kusema kuwa Halmashauri nyingi zinatenga fedha lakini bado hazigusia moja kwa moja wananchi kutatua kero za wananchi , niwaagize kuwa fedha hizo zisitumike kwa matumizi ya kuendesha ofisi bali zitumike katika miradi ya maendeleo
“Sitegemei kuona fedha hizi zinatumika kwa ajili ya matumizi ya ofisi, nategemea fedha hizi zijenge zahanati, madarasa, mabweni, maabara, barabara, masoko, stendi na si kugharamia posho za vikao” amesisitiza Waziri Ummy
Amewaagiza wakurugenzi kuhakikisha wanatumia mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendelo katika Halmashauri zao lengo likiwa ni kutatua kero za wananchi katika maeneo yao
Aidha amesema kuwa mapato na matumizi kwa maendeleo ya wananchi si kazi nyingine