Mradi wa maji uliokataliwa kuzinduliwa na mwenge Mpanda
…………………………………………………………………..
Na. Mwandishi wetu. Katavi
Kiongozi wa mbio maalum za mwenge wa uhuru mwaka 2021 Luteni Josephine Mwambashi amekataa kuzindua mradi wa maji wa IKORONGO II uliopo mtaa wa Mapinduzi katika mtaa wa Mapinduzi katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, wenye uwezo wa kuhudumia watu 32,500
Amekataa kuzindua mradi huo baada ya kutilia shaka gharama za mradi huo ULIOGHATIMU kiasi cha shilingi bilioni 1.7
Akitoa tamko la kukataa kuzindua mradi huo kiongozi huyo wa mwenge kitaifa amesema miundombinu ya mradi huo haitidhishi likiwemo tanki la maji lililogharimu milioni 547 linalodaiwa kupinda na kuwa na nyufa; nyumba ya mlinzi milioni 62 na kibanda cha KUTIBU maji milioni sita
Luteni Mwambashi ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kufuatilia na kukabidhi nyaraka za utekelezaji wa mradi huo kwa uchunguzi zaidi
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amewataka watumishi wa MUWASA kukaa na TAKUKURU na kumpa taarifa za awali kabla mwenge haujaondoka Katavi
Mbunge wa Jimbo la Mpanda mjini Sebastian Kapufi akizungumza katika viwanja vya Kashato amewataka watumishi wanaopewa dhamana ya kusimamia miradi kuchukulia kitendo cha kukataliwa kwa mradi huo kama funzo
Awali Mhandisi wa Mamlaka ya Maji Sagi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Mpanda Mhandisi Edo Richard alisema mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2019 na tanki lake la maji Lina ujazo wa lita milioni moja
Mradi huo ambao tayari umeanza kazi kwa kusambaza maji katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mpanda umesaidia kupunguza mgao wa maji ambapo awali Mpanda ilikuwa ikipata maji kwa asilimia 30 na sasa inapata zaidi ya asilimia 60.