Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani wa Vodacom Tanzania, Brigita Stephen akimuelezea mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam baadhi ya huduma zitolewazo na kampuni hiyo kwenye kampeni ya ‘Kimbiza na 4G ya Ukweli’. Kampeni hiyo ina lengo la kuifahamisha jamii kuhusu kasi na uhakika wa mtandao wake unaowezeshwa na uwekezaji makini katika teknolojia pamoja na upana wa huduma zinazotolewa kwa wateja wake.
Msanii wa kizazi kipya Zena Mohammed maarufu kama Shilole akimuelezea mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam baadhi ya huduma zitolewazo na kampuni hiyo kwenye kampeni ya ‘Kimbiza na 4G ya Ukweli’. Kampeni hiyo ina lengo la kuifahamisha jamii kuhusu kasi na uhakika wa mtandao wake unaowezeshwa na uwekezaji makini katika teknolojia pamoja na upana wa huduma zinazotolewa kwa wateja wake.
