Wawakilishi wa Benki ya Dunia nchini wakiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi Bahati I. Geuzye wakipata maelezo kwa mmoja wa wasimamizi wa kiwanda cha kuunganisha pikipiki za miguu miwili na mitatu mara baada kutembelea moja ya kiwanda cha kuunganisha pikipiki kuangalia baaadhi ya wahitimu wa moja ya Chuo kilichonufaika na mradi unaofadhiliwa na Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) Wawakilishi wa Benki ya Dunia nchini wakiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi Bahati I. Geuzye wakipata maelezo kwa mmoja wa wasimamizi wa kiwanda cha kuunganisha pikipiki za miguu miwili na mitatu mara baada kutembelea moja ya kiwanda cha kuunganisha pikipiki kuangalia baaadhi ya wahitimu wa moja ya Chuo kilichonufaika na mradi unaofadhiliwa na Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF)
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi Bahati I. Geuzye (kushoto) akizungumza jambo na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bi.Xiaoyan Lian mara baada kutembelea moja ya kiwanda cha kuunganisha pikipiki kuangalia baadhi ya wahitimu wa moja ya Chuo kilichonufaika na mradi unaofadhiliwa na Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi Bahati I. Geuzye (Kushoto) akizungumza jambo na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bi.Xiaoyan Lian mara baada kutembelea moja ya kiwanda cha kuunganisha pikipiki kuangalia baadhi ya wahitimu wa moja ya Chuo kilichonufaika na mradi unaofadhiliwa na Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF)
Mmoja wa wasimamizi wa kiwanda cha kuunganisha pikipiki za miguu miwili na mitatu akitoa maelekezo kwa Wawakilishi wa Benki ya Dunia nchini mara baada kutembelea moja ya kiwanda cha kuunganisha pikipiki kuangalia baadhi ya wahitimu wa moja ya Chuo kilichonufaika na mradi unaofadhiliwa na Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) Mmoja wa wasimamizi wa kiwanda cha kuunganisha pikipiki za miguu miwili na mitatu akitoa maelekezo kwa Wawakilishi wa Benki ya Dunia nchini mara baada kutembelea moja ya kiwanda cha kuunganisha pikipiki kuangalia baadhi ya wahitimu wa moja ya Chuo kilichonufaika na mradi unaofadhiliwa na Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF)
Baadhi ya mafundi wakiunganishha pikipiki ya miguu miwili mara baada kutembelewa na Wawakilishi wa Benki ya Dunia nchini kuja kujionea baadhi ya vijana ambao wamehitimu katika moja ya chuo ambacho kinufaika na Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF)
Baadhi ya mafundi wakiunganishha pikipiki ya miguu miwili mara baada kutembelewa na Wawakilishi wa Benki ya Dunia nchini kuja kujionea baadhi ya vijana ambao wamehitimu katika moja ya chuo ambacho kinufaika na Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF)
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*********************************
NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM
Wawakilishi wa Benki ya Dunia nchini wamefanya ziara ya siku moja kukagua miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) unaoendeshwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Mfuko huo unaratibiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ambapo wametembelea moja ya kiwanda cha kuunganisha pikipiki za miguu miwili na mitatu.
Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi Bahati I. Geuzye amesema kupitia ufadhili huo wameona vijana ambapo wamepitia mafunzo katika chuo kilichonufaika na mradi kuendelea kufanya vizuri na kuweza kupata ajira na wengine wakiwa wamejiajiri mtaani.
Amesema kupitia mradi huo kunaongeza upatikanaji wa ajira kwa vijana hasa uwezo wa kujiajiri hasa pale wanapohitimu mafunzo katika vyuo ambavyo ni vinufaiika na miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF).
“Lengo kubwa ya huu mradi ni kuona kwamba vijana wakitanzania zaidi ya elfu 30 mpaka kufikia Juni 2022 wanaweza kupata mafunzo ya ujuzi katika sekta za kipaumbele ikiwemo sekta ya usafirishaji, nishati,Tehama pamoja na utalii”. Amesema Bi.Geuzye.
Kwa upande Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bi.Xiaoyan Lian amesema wamejikita zaidi kuendesha ujuzi ili kuweza kusaidia vijana kupata ajira na kupunguza wimbi la vijana wasio na kazi mtaani.
Nae Mkuu wa Chuo cha Future Word Vocation Institute Bi.Asmin Awadhi amesema wamefanikiwa kupata fedha takribani Milioni 128 ambazo zilitumika katika shughuli nzima za uendeshaji wa mafunzo chuoni ambayo mafunzo yalikuwa ya miezi mitatu.
“Tulifanikiwa kufundisha vijana zaidi ya 400 kati ya hao vijana zaidi ya 80 wameweza kupata ajira katika kampuni mbalimbali na vijana zaidi ya 200 wameweza kujiajiri wenyewe”. Amesema Bi.Asmin.
Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) ni Mfuko unaolenga kufadhili programu za mafunzo ya ujuzi kwa wanufaika 30,000 hadi kufikia mwezi Juni 2022. Mfuko unalenga kufadhili mafunzo ya ujuzi katika sekta sita za kipaumbele ambazo ni Kilimo na Kilimo – Uchumi, Utalii na Huduma za Ukarimu, Uchukuzi, Ujenzi, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Nishati.
Katika awamu ya kwanza ya mradi ulioanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2018/2019 Taasisi 15 zilifadhiliwa kwa jumla ya Shilingi Bilioni 3.1 wakati katika awamu ya pili Taasisi 81 zimenufaika kwa ufadhili wa kiasi cha Shilingi Bilioni 9.7 kuendesha programu za mafunzo ya ujuzi.