Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mashuguru, Kata ya Nanyumbu kuhusu uboreshaji wa huduma ya maji Katika Wilaya hiyo kupitia mradi wa maji wa Mangaka – Nanyumbu.
Mhandisi Sanga amesisitiza eneo hilo ni miongoni mwa maeneo yaliyo katika miradi wa maji wa miji 28.
Utekelezaji wa mradi huo wa Mangaka -Nanyumbu utaondoa adha ya upatikanaji wa huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza,ambapo Serikali itasaini mkataba wa kwa ajili ya kuanza ujenzi ndani ya muda mfupi kuanzia sasa.