Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na wananchi katika Tamasha la Utamaduni la Ngoma za Asili lijulikanalo Tulia ambapo amesema utamaduni wa ngoma za asili utasaidia kukuza utalii hivyo ni vema wananchi wajitokeze kufanya matamasha kama hayo ambayo pia yanaongeza kipato kwa washiriki. Tamasha hilo limefanyika katika Viwanja vya Airport ya zamani jijini Mbeya
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) akimtambulisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) wakati wa Tamasha la Utamaduni la Ngoma za Asili lijulikanalo kama Tulia Traditional Dance Festival lililofanyika leo katika Viwanja vya Airport ya zamani jijini Mbeya.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) akimkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kulia) katika Tamasha la Utamaduni la Ngoma za Asili lijulikanalo kama Tulia Traditional Dance Festival lililofanyika leo katika Viwanja vya Airport ya zamani jijini Mbeya. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini, Dkt. Rashid Chuachua.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akipokea zawadi ya T-shirt kutoka kwa Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) alipotembelea banda la Maryprisca Foundation katika Tamasha la Utamaduni la Ngoma za Asili lijulikanalo kama Tulia Traditional Dance Festival lililofanyika leo katika Viwanja vya Airport ya zamani jijini Mbeya. Anayeshuhudia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb).
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb)(katikati), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kulia) na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) (wa pili kutoka kulia) katika picha ya pamoja na wadhamini waTamasha la Utamaduni la Ngoma za Asili lijulikanalo kama Tulia Traditional Dance Festival lililofanyika leo katika Viwanja vya Airport ya zamani jijini Mbeya.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) wakifuatilia Tamasha la Utamaduni la Ngoma za Asili lijulikanalo kama Tulia Traditional Dance Festival lililofanyika leo katika Viwanja vya Airport ya zamani jijini Mbeya.