KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Pro. Abel Makubi,akizungumza wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya kupimia ugonjwa wa Selimundu zilizotolewa na Taasisi ya General De Pharmacy Limited ya Mkoani Arusha hafla iliyofanyika leo September 23,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Magonjwa yasiyoambukiza Dkt.James Kihologwe,akizungumza wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya kupimia ugonjwa wa Selimundu zilizotolewa na Taasisi ya General De Pharmacy Limited ya Mkoani Arusha hafla iliyofanyika leo September 23,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa General de Pharmacy Lmt. Neville Mushi ,akizungumza wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya kupimia ugonjwa wa Selimundu zilizotolewa na Taasisi ya General De Pharmacy Limited ya Mkoani Arusha hafla iliyofanyika leo September 23,2021 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Pro. Abel Makubi,akiteta jambo na Mkurugenzi wa General de Pharmacy Lmt. Neville Mushi wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya kupimia ugonjwa wa Selimundu zilizotolewa na Taasisi ya General De Pharmacy Limited ya Mkoani Arusha hafla iliyofanyika leo September 23,2021 jijini Dodoma
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Pro. Abel Makubi,akipokea kupokea vifaa vya kupimia ugonjwa wa Selimundu zilizotolewa na Taasisi ya General De Pharmacy Limited ya Mkoani Arusha kutoka kwa Mkurugenzi wa General de Pharmacy Lmt. Neville Mushi hafla iliyofanyika leo September 23,2021 jijini Dodoma
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Pro. Abel Makubi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea vifaa vya kupimia ugonjwa wa Selimundu zilizotolewa na Taasisi ya General De Pharmacy Limited ya Mkoani Arusha hafla iliyofanyika leo September 23,2021 jijini Dodoma
…………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Prof. Abel Makubi amewataka Waganga Wafawidhi katika Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini kuendeleza kampeni ya upatikanaji wa vifaa vya kupimia ugonjwa wa Selimundu katika maeneo yao ili kukabiliana na ugonjwa huo.
Akizungumza leo,Septemba 23,2021 Jijini Dodoma,katika hafla ya kupokea vifaa vya kupimia ugonjwa wa Selimundu zilizotolewa na Taasisi ya General De Pharmacy Limited ya Mkoani Arusha ,Katibu Mkuu huyo amesema gharama za upatikaji wa mashine za kupimia ugonjwa huo zipo juu ambazo ni shilingi milioni 300 mpaka 400.
“Kama tunavyojua ugonjwa wa Selimundu bado ni tatizo hapa nchini inachangia asilimia 6.7 ya vifo vya Watoto chini ya miaka mitano.Vilevile takwimu zinaonesha asilimia 15 hadi 20 ya watanzania wanavinasaba vya Sikoseli hivyo jitihada zinahitajika ili kusaidia mapambano ya ugonjwa huu.
“Natumani hizi mashine ambazo mnazipata ambazo zitaanzia katika Hospitali za Rufaa zitashuka mpaka chini zitasaidia kukabiliana na ugonjwa huu,”amesema Prof.Makubi
Hatahivyo,amewaomba Waganga Wafawidhi katika Hospitali za Rufaa za Mikoa na Wilaya kuendeleza kampeni ya upatikanaji wa vifaa vya kupimia ugonjwa wa Selimundu katika maeneo yao ili kukabiliana na ugonjwa huo.
“Niwaombe waganga wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Wilaya na Mikoa kutoa sapoti ya hii kampeni ya hivi vifaa ambavyo vitasaidia kupima mapema wagonjwa ambao wana sikoseli.Nitoe rai kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kutoa misaada mbalimbali katika sekta ya afya ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi,”amesema.
Vilevile.Prof. Makubi amesema anatamani kuwe na kituo cha kukabiliana na ugonjwa huo hususani Mikoa yenye tatizo hilo hivyo amewaomba wadau wenye uwezo kusaidia jambo hilo.
“Lakini pia nilikuwa natamani wadau wetu tunahitaji kujenga ‘centre’ ya kukabiliana na ugonjwa wa Sikoseli hapa nchini nipendekeze wadau wenye uwezo basi tushirikiane hususan mikoa ambayo ina tatizo zaidi,”amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa General de Pharmacy Lmt. Neville Mushi amesema kuwa vifaa walivokabidhi vimegharimu shilingi Millioni 28.
“Lengo la kukabidhi vifaa ni baada ya kusikiliza hotuba nyingi katika maadhimisho ya siku ya Selimundu duniani kuona kuwa tatizo hili ni kubwa sana Nchini,”
“Tulipokea maombi kutoka kwa chama Cha selimundu Tanzania wao walianza kuomba mashine mbili lakini sie kwa namna ya kipekee tulivoguswa tuliamua kuwapatia mashine 5 pamoja na vipimo vya test vya 50 kwa 50,”alisema Mkurugenzi
Aidha, amesema kuwa kipimo hicho hakitakuwa kikipima selimundu pekee bali kinauwezo wakupima magonjwa mengine pia kama Maralia,HIV pamoja na UVIKO-19.
Naye,Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ambaye alimwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt.James Kihologwe amesema kwa sasa Serikali ina vituo vitano ambavyo vinapima ugonjwa wa Selimundu hivyo wamejipanga kuhakikisha huduma ya upimaji inakuwa karibu na mwananchi.
Amesema takribani asilimia 6.7 ya vifo vya watoto wachanga vinatokana na ugonjwa wa Selimundu na takribani asilimia 15 mpaka 20 ya watanzania wanavinasaba vya ugonjwa huu na kila mwaka watoto 11,000 wanazaliwa wakiwa na tatizo la ugonjwa huo.
“Kwa hiyo tunataka huduma hizi zifike karibu na wananchi nini cha kufanya ni kuhakikisha vifaa vinafika hii ni chachu tu kuonesha katika hospitali zetu ni rahisi kuwafikia lengo letu ni kuhakikisha watu wengi zaidi wanapimwa kama wanavinasaba vya ugonjwa wa selimundu,”amesema.