***
Wawakilishi wa vikundi vya wajasiriamali kutoka kutoka vijiji vinayozunguka mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, uliopo katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, wanashiriki katika maonesho ya tatu ya Wajasiriamali kitaifa yanayoendelea katika wilaya ya Kasulu kwa ufadhili wa kampuni hiyo ambayo yataisha Septemba 30, 2021.
Maonesho hayo ambayo yamewakutanisha wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali nchini yameandaliwa na Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma na yalizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.
Lengo la maonesho hayo ni kutoa fursa ya kupanua wigo wa masoko ya bidhaa zinazzalishwa na viwanda vidogo,kubadilishana ujuzi na uzoefu kwa wanajisriamali na wanaviwanda pamoja na kuonesha teknlojia mbalimbali zinazozalishwa hapa nchini.
Akiongea kwa niaba ya wajasiriamali wenzake waliowezeshwa na Barrick kushiriki katika maonyesho hayo, Clementina Felix , anayejishughulisha na ushonaji na ubunifu wa mavazi aliishukuru Barrick Bulyanhulu, kwa kuwawezesha kushiriki maonyesho hayo makubwa ambayo yatawawezesha kujifunza mambo mbalimbali yatakayowawezesha kukuza biashara zao.
“Kupitia maonesho haya tutaweza kupata fursa ya kuonesha bidhaa tunazozalisha pia tutaweza kupata elimu ya kufungasha bidhaa, urasimishaji biashara na kufungua fursa zaidi za masoko, tumekuja na bidhaa zaidi ya 100 za kuonesha”, alisema Felix.
Aliongeza kusema kuwa miongoni mwa wajasiriamali waliowezeshwa na kampuni ya Barrick, wanajihusisha na kilimo cha mazao ya nafaka, mbogamboga na matunda, wafugaji wa kuku na nyuki, washonaji wa nguo na kutengeneza mazuria na viatu.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano na Jamii wa Mgodi wa Barrick wa Bulyanhulu, Antony Sebastian, alisema wajasiriamali hawa ni sehemu ya shughuli za maendeleo ya mgodi wa Bulyanhulu ambao wanawezeshwa kupewa elimu ya ujasiriamali na kwa wale wanaojishughulisha na kilimo wanapatiwa mbegu, mbolea na dawa za kuulia wadudu ili wafanikiwe kuendesha kilimo cha kibiashara.
Sebastian ameishukuru SIDO kwa kuandaa maonyesho haya yaliyowakutanisha wajasiriamali na wadau mbalimbali wa sekta ya ukuzaji wa biashara ndogondogo .
Wajasiariamali wanaowezeshwa na kampuni ya Barrick wakionesha bidhaa zao wanaozalisha
Wajasiariamali wanaowezeshwa na kampuni ya Barrick wakionesha bidhaa zao wanaozalisha
Wajasiariamali wanaowezeshwa na kampuni ya Barrick wakionesha bidhaa zao wanaozalisha
Wajasiriamali kutoka Kahama wanaowezeshwa na Barrick wakiwa katika picha ya pamoja kwenye maonesho ya Kasulu