Makamu Mwenyekiti wa bodi ya benki ya biashara ya DCB ,Zawadia Nanyaro akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya ukaguzi wa ndani unaofanyika jijini Arusha.
Mjumbe wa bodi ya IIA ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Africanmark services, Berthasia Ladislaus akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kwenye mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya ukaguzi wa ndani.(Happy Lazaro).
………………………………………………………………………….
Happy Lazaro,Arusha.
Aliyekuwa Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali CAG ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Wajibu ,Ludovic Utoh amesema kuwa,kuna umuhimu mkubwa Sana wa kuwepo kwa swala la uwajibikaji katika taasisi na makampuni mbalimbali ili kuweza kuleta maendeleo katika nchi yetu.
Ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa nane wa wakuu wa Taasisi za serikali na binafsi wenye mada kuu ya uwajibikaji katika kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla ulioandaliwa na Taasisi ya ukaguzi wa ndani unaofanyika mjini hapa.
Amesema kuwa,kuna umuhimu mkubwa sana wa kuwepo kwa uwajibikaji katika sehemu mbalimbali ili ziweze kuleta maendeleo katika maeneo husika.
“Nawashukuru Sana Taasisi hii ya wakaguzi wa ndani kwa kuandaa mkutano huu ambao unalenga kukumbushana na kuelimishana katika kuangalia uwajibikaji na nafasi ya wakaguzi wa ndani katika kuleta maendeleo yetu na ya nchi kwa ujumla kwani kila mmoja wetu anatambua kuwa hakuna maendeleo yanayoweza kuja bila uwajibikaji mahali popote.”amesema .
Utoh amesema kuwa,kupitia mkutano huo wanaangalia umuhimu wa uwajibikaji na maendeleo katika nafasi ya taaluma ya ukaguzi ili kujua wao wanahusikaje kwa sababu nchi inalilia sana maendeleo na watanzania wanahitaji Sana maendeleo .
Amefafanua zaidi kuwa,watu wengi Sasa hivi wanaona umuhimu wa wakaguzi wa ndani kwani wapo kuwashauri na kuwalekeza wasimamizi na wakuu wa mashirika na Taasisi katika kufanya vizuri kwenye utendaji kazi wao.
Mmoja kati ya waandaji wa tamasha hilo,Zelia Njeza amesema kuwa,lengo la tamasha hilo ni kutoa elimu kwa wakuu wa Taasisi mbalimbali za serikali na binafsi ambapo kwa mwaka huu wanalenga kutoa elimu juu ya uwajibikaji na utawala bora katika maendeleo ya Taasisi na Taifa kwa ujumla.
“lengo la kutoa elimu hii ni kuhakikisha wakurugenzi wa bodi mbalimbali Tanzania tunawawezesha kutoa huduma vizuri ,huku dhana kuu ya uwajibikaji kwa maendeleo mapana ya taasisi na nchi kwa ujumla.”amesema Njeza.
Amefafanua kuwa,wamefikia hatua ya kutoa mafunzo hayo kwa lengo la kukumbushana utendaji kazi wao kwani ili uweze kuwa kiongozi mzuri lazima uendelee kujifunza kila siku kulingana na mabadiliko ya teknolojia na hatimaye kuweza kuwa wakuu wanaotambulika sio Tanzania tu hata duniani kwa ujumla.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya biashara ya DCB ,Zawadia Nanyaro amesema kuwa,mkutano huo unajumuisha wajumbe wa bodi na wanaosimamia kamati.za ukaguzi ambapo alisema ni mkutano muhimu Sana kwa wakurugenzi wa bodi mbalimbali kwani wanaweza kupata taarifa na mafunzo namna ya kusimamia kampuni zao .
Amesema kuwa,bodi ya uongozi ndo ina mamlaka hivyo kupitia mafunzo hayo viongozi hao wanapata fursa ya kujifunza na kuongea katika vikao vyao.
Naye Mjumbe wa bodi ya IIA ,Berthasia Ladislaus amesema kuwa,lengo ni kutoa elimu endelevu katika ukaguzi kwenye utawala bora na uwajibikaji kwa wadau kutoka Serikali na Taasisi binafsi .
Amesema kuwa,wanakutana kubadilishana mawazo katika uwajibikaji na maendeleo kwani wakaguzi wa ndani wana mchango mkubwa Sana katika maendeleo ya nchi na Taasisi hivyo ili kuwasaidia lazima kuwepo na mafunzo kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao na hatimaye Taasisi zao ziweze kuwa salama zaidi.
Amefafanua kuwa,wanapozungumzia swala zima la maendeleo lazima watu wafahamu na wasimamie katika kuona rasilimali zinatumika upasavyo ili kufikia malengo yaliyowekwa kwani bila kuwepo kwa wakaguzi wa ndani huenda rasilimali zisitumike ipasavyo.