Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi ACP Benjamin Kuzaga aliyeshika PIKIPIKI akimuonesha Mkuu wa mkoa Katavi Bi. Mwanamvua Mrindoko pikipiki zilizopatikana baada ya kuibiwa
Baadhi ya vitu vilivyoibiwa na kupatikana zikiwemo sofa, magoforo na meza ya kioo
………………………………………………………………………
Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi limewakamata watu 19 kwa tuhuma za uvunjaji wa nyumba na wizi wa vitu mbalimbali vya matumizi ya nyumbani zikiwemo runinga, radio, feni, sofa set, pikipiki, magodoro, rice cooker, majiko ya gesi na jenereta katika operesheni maalum ya siku tatu ya kuondoa vibaka iliyofanyika katika manispaa ya mpanda; ambapo watuhumiwa wengine wamekatwa katika mikoa ya kigoma na tabora
Akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Katavi; Kamanda wa Polisi mkoa Benjamin Kuzaga amesema wamefanya operesheni maalum ya siku tatu na kubaini watu hao wanashirikiana na wa mikoa jirani katika uuzaji wa vitu hivyo
Ameongrza kuwa watu 15 wamekamatwa katika manispaa ya Mpanda na wengine wanne wamekamatwa katika mikoa ya Tabora na Kigoma
Kamanda Kuzaga ameeleza kuwa katika kamata kamata hiyo pia wamewakamata mafundi wa TV na pikipiki pamoja na madalali wanaojihusisha na vitendo hivyo viovu
“Tumekata chain hii nzima nab ado tunaendelea mpka mkoa wa Rukwa, lengo kubwa ni kuhakikisha mji wetu unakuwa na Amani na hawa walioshindwa tabia wanavuruga maendeleo ya wananchi tutahakikisha tunawakomesha” alisema
Amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani ili sharia ichukue mkondo wake
Aidha kamanda Kuzaga amekemea tabia ya kuficha wahalifu na kutoa wito kwa jamii kutoa taarifa ili kusaidia kukomesha tabia za wizi
Akizungumzia tukio hilo mkuu wa mkoa wa Katavi Bi. Mwanamvua Mrindoko amewataka viongozi wa vijiji na mitaa kutowafumbia macho watu wenye tabia za uovu
Bi. Mrindoko amesema kamati ya ulinzi na usalama mkoa haitavumilia tabia hiyo kwani wizi mdogo mdogo umezidi na kutaka wafikishwe mahakamani kwa hatua za kisheria