Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SGA Security, Eric Sambu (kulia) akiwa na baadhi ya wadhamini wa NMB Marathon 2021. SGA ni moja wa wadhamini wa mbio hizo zenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kutibu wanawake wenye Fistula katika hospitali ya CCBRT.
Wafanyakazi wa SGA Security wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mbio za majaribio za NMB Marathon 2021 katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam. SGA ni moja wa wadhamini wa mbio hizo zenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kutibu wanawake wenye Fistula katika hospitali ya CCBRT.
************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SGA Security ambayo ni moja ya makampuni ya ulinzi yanayoongoza nchini imetangaza kuwa itaendelea kudhamnini michezo nchini.
Akizungumza Jijni Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SGA Security, Eric Sambu alisema kampuni hiyo inadhamini NMB Marathon 2021 ambayo itafanyika Jumamosi ya wiki hii katika Viwanja vya Leaders Club na yenye lengo ya kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya wanawake wenye Fistula katika hospitali ya CCBRT.
“SGA inaamini michezo ni muhimu kwa jamii yenye afya bora ambayo ni chachu kubwa ya maendeleo ya taifa,” alisema.
Alisema udhamini huu ni sehemu ya mkakati wa SGA kuchangia katika huduma za kijamii huku ikitenga asilimia moja ya mauzo kwa huduma za kijamii kama hizi.
Katika hatua nyingine, amesema pia SGA imedhamini tamasha la michezo la wanawake la Tanzanite (Tanzanite Women Sports Festival 2021) lililofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuwakusanya zaidi ya wanamichezo 5000 wa kike mwishoni mwa wiki.
Tamasha hilo liliandaliwa na Wizara ya Michezo na Utamaduni kama ilivyoelekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan. SGA ilitoa ulinzi na huduma ya kwanza na zimamoto.
Alisendelea kusema kuwa mwezi ujao kampuni hiyo pia itadhamini mbio za NBC Capital City huu ukiwa ni mara ya pili mfulululizo.
Aidha, alisema kampuni hiyo imedhamini safari maalumu ya baiskeli ijulikanayo kama ‘the Great African Cycling safari’ itakayoshirikisha nchi tano za Afrika Mashariki ambayo ilianzia Jijini Dar es Salaam Agosti 1 na kuingia nchini Kenya kupitia Tanga, kisha kuelekea Mombasa, Nairobi, Kampala, Kigali, Bujumbura, Dodoma na hatimaye kumalizikia Arusha ambayo ndio makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Safari hiyo ni ya kilomita 6000 hadi mwisho na itachukua takriban siku 55. SGA ilivutiwa na kauli mbiu ya safari hiyo ya kuwa na Jumuiya moja, kuondoa vikwazo katika biashara na kuwaunganisa wana Afrika Mashariki.
Kwa upande wa mpira, Bw. Sambu alisema wamekuwa wakisaidia academy mbalimbali za ndani kukuza vipaji kwa kuwapa vifaa vya michezo na kuwafundisha masuala ya kiusalama na afya. Miongoni mwa mashirika yaliyodhaminiwa na SGA ni lile la Magnet (Magnet Youth Sports Organisation) ambalo limeshapeleka vijana katika academyza ulaya.
Baadhi ya vijana hawa ni Baraka Seif aliyekuwa Ajax, Amsterrdam na wengine wako Celta Vigo kule Uspania na Leicester ya Uingereza.
Bw. Sambu alisema mchango huu wa SGA katika shughuli mbalimbali za kimichezo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya shughuli za kampuni hiyo Afrika Mashariki.
SGA Security ina magari zaidi ya 800 katika ukanda huu. “Tunasafiri zaidi ya km 12,000 kila siku kuimarisha biashara katika ukanda huu. Katika kila shilingi inayoguswa Afrika Mashariki angalau senti 80 huwa imesafirishwa na SGA,” alisema na kuongeza kuwa SGA imeajiri zaidi ya wafanyakazi 19,000 katika Jumuiya ya Afrika Mashariki hivi kuifanya kampuni kubwa zaidi ya ulinzi.
SGA Security inatoa huduma mbalimbali ikiwemo za ulinzi, alarm, huduma za fedha, ulinzi wa kielektroniki, huduma ya kusafirisha mizigona huduma nyinginezo na ndio kampuni pekee ya ulinzi yenye cheti cha ISO 18788 – Security Operations Management System.
Mwaka huu kampuni hiyo ilipokea tuzo baada ya kutangazwa mshindi wa jumla kama kampuni yenye rasilimali za kutosha na ya kuaminika (Most Equipped and Reliable Security Company of the Year, 2020) katika tuzo za chaguo la wateja (Consumer Choice Award).