Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kushoto) akisalimia leo na viongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Mjini Tabora (TUWASA) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea miundombinu ya maji ya TUWASA.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kushoto)akiongozana na viongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Mjini Tabora (TUWASA) leo kukagua Bwawa na Maji la Igombe alipokuwa kwenye a ziara yake ya kikazi ya kutembelea miundombinu ya maji ya TUWASA.
Meneja ufundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Mjini Tabora (TUWASA) Juma Kasekwa (wa pili kutoka kulia) akitoa maelezo leo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (katikati) jinsi mitambo inavyofanya kazi ya kuvuta maji kutoka Bwawa la Igombe na kupeleka kwenye eneo la kuyasifisha.
Kaimu Mkurugenzi Mteandaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Mjini Tabora(TUWASA )Mayunga Kashilimu(wa pili kutoka kulia) akitoa maelezo leo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea miundombinu ya maji ya TUWASA.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kushoto)akiwa na viongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Mjini Tabora (TUWASA) akitoka kukagua Bwawa na Maji la Igombe leo alipokuwa kwenye a ziara yake ya kikazi ya kutembelea miundombinu ya maji ya TUWASA.
Meneja ufundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Mjini Tabora (TUWASA) Juma Kasekwa (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (wa kutoka kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt Yahya Nawanda ( wa tatu kutoka kushoto) kuhusu mnara wa ujenzi wa Bwawa la Igombe walipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya kutembelea miundombinu ya maji ya TUWASA.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani akiangalia eneo ambao tope linatolewa kwenye matenki ya maji yaliyopo katika Bwawa la Igombe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea miundombinu ya maji ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Mjini Tabora (TUWASA.)
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani akizungumza na baadhi ya watumishi na viongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Mjini Tabora (TUWASA) leo baada ya kukagua Bwawa na Maji la Igombe alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kutembelea miundombinu ya maji ya TUWASA.
Meneja ufundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Mjini Tabora (TUWASA) Juma Kasekwa (wa kushoto) akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (katikati) leo mmoja ya chemba ambayo inapokea maji ya mradi wa ziwa Victoria kwa ajili ya kuyapeleka Tenki kuu la Itumba lilipo katika Manispaa ya Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kushoto) akitoka kukagua Tenki la maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria la Itumba katika Manispaa ya Tabora leo alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea miundombinu ya maji ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Mjini Tabora (TUWASA)
…………………………………………………………………………………
NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewataka wananchi na Taasisi zote zinazodaiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi na Mazingira Mjini Tabora (TUWASA) kulipa bili zao ili fedha zitakazopatikana zisaidie kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji safi na salama wananchi wengi.
Alisema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kila mwananchi na anafikiwa na huduma ya majisafi na salama nyumbani kwake na wengine wapata huduma hiyo katika vituo vilivyo karibu na nyumba zao.
Balozi Dkt. Batilda ametoa kauli hiyo leo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea miundombinu ya maji ya TUWASA.
Alisema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imekusudia ifikapo mwaka 2025 kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wananchi wote wanapata huduma ya majisafi na salama majumbani mwao.
Balozi Dkt. Batilda alisema Serikali inaendelea kujenga miundombinu ya maji na kutoa fedha kwa ajili ya shughuli za kumtua ndoo mwanamke na hivyo ni vema kila mtumiaji maji atimize wajibu wake wa kulipia Ankara kila zinapotolewa.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema atajitahidi kukutana na Taasisi za Umma zinazodaiwa na TUWASA ili waweze kueleza mpango wa kulipa madeni yao na kuwawezesha kuendeleza kazi nzuri ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wakazi wote kuwa walinzi wa miundombinu ya maji na kuwafichua waharibifu wa mazingira ambavyo ndio vyanzo vya maji.
Alisema tatizo la uchomaji moto mkoani Tabora ni kubwa ni vema Kamati za Mazingira ndani ya vijiji zikatekeleza wajibu wao kwa kuwakamata watu wote wanaochoma moto ovyo na wale wanaolima ndani ya vyanzo vya maji na wanaoendesha shughuli za kibinadamu kinyume cha Sheria.
Kaimu Mkurugenzi Mteandaji wa TUWASA Mayunga Kashilimu alisema baadhi ya wateja wao hasa Taasisi za umma wamekuwa wakitumia huduma ya maji bilia kulipia matumizi yao kwa wakati ambapo hadi hivi sasa wanadaiwa kiasi cha shilingi bilioni 1.
Alisema hali hiyo imesababisha kukwama kwa baadhi ya shughuli za kuongeza miundombinu ya maji safi na salama kwa wateja wao.
Kashilimu alimuomba Mkuu wa Mkoa kuwasaidia kuzikumbusha Taasisi hizo ili fedha hizo iwasaidie katika kuendeleza kazi ya kuboresha miundombinu.
Aidha, alisema Serikali imetenga jumla ya shilingi milioni 600 kwa ajili ya kuanza kuboresha huduma ya maji kwenye Miji ya Sikonge na Urambo.
TUWASA inahudumia wilaya ya Tabora Uyui Sikonge Urambo na Kaliua.