Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Mgama akiongelea maswala ya ramri chonganishi ambazo zinachochea migogoro kwa wananchi wa kata hiyo
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Bashir Muhoja akiongea na wananchi wa kata ya Mgama akiongelea maswala ya ramri chonganishi ambazo zinachochea migogoro kwa wananchi wa kata hiyo
Baadhi ya wananchi wakiwasikiliza viongozi kutoka wilaya ya Iringa walipofika kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Baadhi yawananchi katika Kijiji Chai Itwaga wilayani Iringa wameilalamikia Serikali kwa kushindwa kuwadhibiti waganga wa asili wanaopiga ramri chonganishi na kuibua uhasama unaohatarisha amani katika jamii.
Wakizungumza katika Mkutano wa hadhara baadhi ya Wananchi hao walisema hali ya usalama katika Kijiji hicho imekuwa ndogo kutokana na waganga kuwaaminisha wananchi juu ya Ushirikiana uliokithiri huku Serikali ikiendela kukaa kimya pasipo kuwakemea.
Walisema kuwa kumekuwa kukitokea kwa matukio mengi kijijini hapo na yote yamekuwa yakihusiswa na imani za kishirikina jambo linalochangia kuwaita waganga wa kienyeji kutoka nje ya kijiji hicho kwenda kufanya ramri chonganishi kwa wananchi.
Wananchi hao walisema kuwa hivi karibuni kulitokea ajali ya pikipiki kugongana na kusababisha vifo kwa wananchi wa kijiji hicho jambo ambalo nalo lilichukuliwa kama ajali iliyotokana na maswala ya ushirikina.
Walisema kuwa waganga hao wa jadi ambao wamekuwa wakifika kijijini hapo na kupiga ramri chonganishi wamekuwa wakifanya kazi bila ya kuwa na kibali maalum kutoka serikali na kujifanyia mambo wanayokata kwa kuchochoe uhasama kwa wananchi.
“Hivi tunaomba kuuliza kuwa kweli serikali ya kijiji ipo au maana waganga hawa wa kienyeji wamekuwa wanaingia kijijini hapa na kufanya shughuli ya kupiga ramri chonganishi na serikali imekuwa haiwachukulii hatua yoyote ile eti viongozi kutoka wilayani unalikubali hilo?” walisema wananchi.
Awali akitoa taarifa kwa niaba ya mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Iringa Joel Msiba ambaye ni mpelelezi wa tarafa ya Kiponzero na …..alisema kuwa kijijini hapo kumekuwa na imari za kishirikiana kwa kuwaita waganga wa kienyeji kuwanywesha dawa za kienyeji ambazo zimekuwa zikichochea ugomvi baina ya wananchi na wananchi.
Alisema kuwa hivi karibu kulitokea ajali ya pikipiki katika kijiji hicho na kupelekea wanananchi kuwaleta waganga wa kienyeji kupiga ramri chonganishi ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo kwa wananchi .
Afande msiba alisema kuwa wananchi wamekuwa wakitoa kiasi cha pesa zaidi ya shilingi laki saba kwa ajili ya kulipia ramri kwa waganga jambo ambalo limekuwa likichangia uchonganishi kwa jamii inayoishi katika kijiji hicho.
Alimalizia kwa kuwataka wananchi wa kijiji cha Itwaga kuacha mara moja tabia hiyo ambayo imekuwa ikiwachonganisha wananchi lakini imekuwa ikididmiza uchumi wa wananchi kwa kutoa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya waganga badala ya pesa hiyo kufanyia shughuli nyingine za kimaendeleo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Bashir Muhoja alisema kuwa ni kosa kubwa kwa mtendaji wa kata,kijiji kumruhusu mganga wa kienyeji kufanya kazi yoyote kwenye kijiji au kata bila ya kuwa na kibali maalum kutoka kwa viongozi husika.
Alisema kuwa waganga wa kienyeji hawarusiwi kufanya kazi yeyote ile kijijini bila kuwa na kibali hivyo ikitokea mtendaji yoyote yule ameruhusi jambo hilo bila kibali maalum basi mtendaji huyo atachukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria kwa mujibu wa mkataba wake wa ajira serikalini.
Naye mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa swala la ramri chonganishi haliruhusiwi kwa kuwa limekuwa linahatarisha usalama wa wananchi kwa kuwa hata serikali hailikubari swala hilo.
Alisema kuwa ni marufuku kupiga ramri chonganishi katika vijiji au kata hivyo watendaji wote marufuku kutoa kibali chochote kile kwa ajili ya kufanya ramri chonganishi kwa kuwa swala hilo limekuwa likichochea migogoro kwa wananchi.
Moyo alisema kuwa ni marufukuwa kwa watendaji wote wa wilaya ya Iringa kutoa vibari kwa ajili ya ramri chonganishi katika wilaya hiyo kwa lengo la kuondoa migogoro ya wananchi inayotokana na hizo ramri changanishi.