Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani akizungumza kwa niaba ya Afisa Elimu Mkoa wa Singida wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa walimu walezi wa watoto wanaohudumiwa na Taasisi ya Social Action Trust Fund (SATF) ilioandaa mafunzo hayo yaliyofanyika leo Kanda ya Kati na kuhusisha mikoa ya Pwani, Morogoro, Arusha, Dodoma na Singida.
Mratibu wa Taasisi hiyo kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
( TAMISEMI) Idara ya Elimu Dkt. Johanes Balige akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Meneja Miradi wa taasisi hiyo Nelson Rutabanzibwa akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Afisa Programu Ufuatiliaji na Tathmini wa Taasisi hiyo Helen Kilontsi akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
Mfanykazi wa Taasisi hiyo Joselina Mutoka akiwajibika.
Mratibu Mtaalam wa Miradi wa Taasisi hiyo Edgar Kihwelo akitoa mada kwenye mafunzo hayo.
Mnufaika wa taasisi hiyo Habel Kenneth kutoka Dodoma akizungumza kwenye mafunzo hayo jinsi Taasisi hiyo ilivyomsaidia kupata elimu.
Mwalimu Nickson Sanga kutoka Kondoa Dodoma akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mwalimu Boniface Lyoka kutoka Kondoa Dodoma akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo kwa vitendo yakifanyika.
Mwalimu Jenitha Dismas kutoka Kondoa Dodoma akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo kwa njia ya makundi yakifanyika.
Mwalimu Upendo Chenga kutoka Wilaya ya Arusha DC akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo kwa njia ya makundi yakifanyika.
Na Dotto Mwaibale, Singida
TAASISI ya Social Action Trust Fund (SATF) iliyoanzishwa kwa udhamini wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Serikali ya Marekani (USAID) na kuratibiwa na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kusaidia juhudi za Serikali katika kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kupunguza athari zitokanazo na ugonjwa wa Ukimwi hapa nchini limetoa mafunzo ya siku moja kwa walimu walezi wa watoto wanaohudumiwa na taasisi hiyo Kanda ya Kati yaliyohusisha mikoa ya Pwani, Morogoro, Arusha, Dodoma na Singida.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Afisa Elimu Mkoa wa Singida, Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani alisema wajibu wa kumlinda mtoto ni wa kila mwanajamii lakini walimu wanawajibu mkubwa kwa kuwa wanakaa na watoto hao kwa muda mrefu hivyo wanapaswa kuwalinda wakiwa katika mazingira ya shule na nje ya shule.
Alisema pia walimu wanawajibu wa kulinda maadili na utamaduni wa watoto ukizingatia kuwa hivi sasa kuna utandawazi na matumizi ya mitandao mbalimbali ya kijamii hivyo bila kuwalinda wanaweza kuharibika kwa kuiga utamaduni wa nje na kupotosha utamaduni wetu.
“Nitoe wito kwenu walimu katika mazingira yenu ya kufundisha mjikite zaidi katika kulinda utamaduni na maadili yetu ya kitanzania,”.alisema Ndahani.
Aliwata walimu hao kuwa wazalendo kwani hawawezi kuwalinda watoto bila ya kuwa na uzalendo wa nchi ukizingatia kuwa wao ndio wanakaa na watoto hao kwa muda mrefu kuliko mtu mwingine.
Mratibu wa Taasisi hiyo kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
( TAMISEMI) Idara ya Elimu Dkt. Johanes Balige alisema Serikali imekuwa ikishirikiana na taasisi hiyo katika kuiongoza kwa kufanya shughuli zao kwa kuzingatia miongozo iliyowekwa na kuwa ni taasisi ambayo inafanya kazi zake vizuri.
Meneja Miradi wa taasisi hiyo Nelson Rutabanzibwa alisema taasisi hiyo ilianza mwaka 1998 na kuwa tangu ianze kufanya kazi walikuwa na bajeti ndogo ilioanzia Sh. milioni 500 kwa mwaka kwa ajili ya miradi ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Alisema lakini mpaka hivi sasa bajeti yao imeongezeka hadi kufikia Sh.1 Bilioni na kuwa watoto zaidi ya 200,000 wamefikiwa kwa kupewa msaada wa elimu na huduma za afya.
Alisema wametoa mafunzo ya namna hiyo kwa walimu walezi 150 ambao wanafanya nao kazi katika mikoa 16 ya Tanzania Bara na Halmashauri za wilaya 34 na kuwa mafunzo hayo yamefanyika kikanda kuanzia Kanda ya Kusini, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kati ambapo yamefikia tamati leo.
Mwalimu Upendo Chenga kutoka Wilaya ya Arusha DC alisema mafunzo hayo yatawasaidia kuwalea watoto wanaosaidiwa na taasisi hiyo kwa kupatiwa ufadhili kuanzia ngazi ya chini hadi elimu ya juu.
Mwalimu Samuel Imbori kutoka Wilaya ya Ikungi aliiomba taasisi hiyo kuongeza idadi ya watoto wanaopatiwa msaada huo waliopo wilayani humo kutoka saba hadi 15 ukizingatia changamoto ya watoto wenye mahitaji kuwa kubwa.
Alisema watoto hao wanaosaidiwa na taasisi hiyo wamekuwa wakifanya vizuri katika masomo yao ukilinganisha na awali kabla ya kupata msaada huo.
Mratibu wa Shirika la Oblige for Valnerable Children Tanzania (OVCT) lenye Makao Makuu Puma wilayani Ikungi mkoani hapa, Benard Sungi ambao wanafanya kazi kwa kushirikiana na taasisi hiyo alisema kwa ushirika wao wameweza kufanya kazi katika Kata nne za Ihanja, Lighwa, Isunna na Kituntu ambapo waliwabaini watoto 80 ambao walikuwa katika mazingira magumu ambao wamepata ufadhili wa masomo kupitia Taasisi hiyo ya SAFT.
Mnufaika wa taasisi hiyo Habel Kenneth kutoka Dodoma ambaye ametoka katika kaya masikini alisema alianza kufadhiliwa na SATF akiwa kidato cha pili hadi chuo kikuu ambapo alipata digrii yake ya kwanza na sasa ameajiriwa amejenga nyumba, ameoa na ana mtoto mmoja.