Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Gerald Mweli akiongoza kikao cha Wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Maji na Wakurugenzi wa Halmashauri za Magu, Nzega, Mkalama na Kondoa wanaotekeleza Mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika maeneo kame, mradi unaosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais. Wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis Abdullah. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Dodoma.
Wakurugenzi wa Halmashauri za Magu, Nzega, Mkalama na Kondoa pamoja na Wanasheria wao wakionyesha hati za makubaliano kati ya Halmashauri zao na RUWASA kuhusu uchimbaji wa visima, mabwawa madogo, malambo na ujenzi wa miundombinu ya uvunaji maji ya mvua katika katika Halmashauri zao. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos na Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Daudi Makendi wakipitia vipengele vya Hati ya Makubaliano baina ya Halmashauri yao na RUWASA katika kusimamia uchimbaji wa visima, mabwawa madogo, malambo na ujenzi wa miundombinu ya uvunaji maji ya mvua
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Bi. Fidelica Myovela na Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Merchades Rusasa wakisaini Hati ya Makubaliano baina ya Halmashauri yao na RUWASA katika kusimamia uchimbaji wa visima, mabwawa madogo, malambo na ujenzi wa miundombinu ya uvunaji maji ya mvua
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. rchanus Kilajo na Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Mashauri Vicent wakisaini Hati ya Makubaliano baina ya Halmashauri yao na RUWASA katika kusimamia uchimbaji wa visima, mabwawa madogo, malambo na ujenzi wa miundombinu ya uvunaji maji ya mvua
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Bw. Kiomoni Kibamba na Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Stephen Nyagalu wakisaini Hati ya Makubaliano baina ya Halmashauri yao na RUWASA katika kusimamia uchimbaji wa visima, mabwawa madogo, malambo na ujenzi wa miundombinu ya uvunaji maji ya mvua