Home Siasa LENGO LA SERIKALI NI KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO

LENGO LA SERIKALI NI KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO

0

Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme akihutubia wakazi wa shina namba 3 tawi la Mchemo, Kata ya Mchemo, Wilaya ya Newala, mkoani Mtwara ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM yenye lengo la kukagua, kusimamia na kuhamasisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025. (Picha na CCM Makao Makuu)


Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme leo amefanya ziara katika wilaya ya Newala mkoani Mtwara ikiwa ni sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa yenye lengo la kukagua, kusimamia na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 – 2025.
Naibu Katibu Mkuu amefanya vikao vitatu katika shina namba 3 Kitangari shina namba 3 Mchemo na Wazee wa Wilaya ya Newala.
Ndugu Mndeme pia ametembelea miradi miwili katika wilaya hiyo ambapo alitembelea Shule ya Sekondari Mpotola yenye idadi ya wanafunzi 766 ambapo amekagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, ofisi na maabara pamoja na maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Newala
“Lengo la Serikali ni kupunguza vifo vya mama na mtoto na Serikali yetu ya awamu ya sita imefanikiwa kupunguza vifo vya wajawazito, vifo vya watoto wa umri wa chini ya miaka 5”
Alisema Ndugu Mndeme wakati akizungumza na wananchi, hospitali hii imepokea fedha kwa awamu mbili jumla ya Tshs. 1,500,000,000/= na inatarajiwa kuhudumia  wananchi wa Newala,Tandahimba, Masasi na Mtama.