Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ,Remidius Emanuel,akizungumza wakati wa kufungua kongamano la maendeleo ya Wilaya ya hiyo lililoshirikisha wadau mbalimbali wa kutoka ndani na nje ya wilaya hiyo lilofanyika ukumbi wa chuo cha ufundi Veta.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ,Dk Omari Mkulo,akizungumza wakati wa kufungua kongamano la maendeleo ya Wilaya ya hiyo lililoshirikisha wadau mbalimbali wa kutoka ndani na nje ya wilaya hiyo lilofanyika ukumbi wa chuo cha ufundi Veta.
Baadhi ya washiriki wakifatilia kongamano la maendeleo ya Wilaya ya hiyo lililoshirikisha wadau mbalimbali wa kutoka ndani na nje ya wilaya hiyo lilofanyika ukumbi wa chuo cha ufundi Veta.
Spika wa Bunge ,Job Ndugai akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ,Remidius Emanuel,wakikagua mabanda wakati wa kongamano la maendeleo ya Wilaya ya hiyo lililoshirikisha wadau mbalimbali wa kutoka ndani na nje ya wilaya hiyo lilofanyika ukumbi wa chuo cha ufundi Veta.
………………………………………………………………………….
Na.Mwandishi Wetu,Kongwa
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa ,Remidius Emanuel amewataka wananchi kushirikiana katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya kiuchumi katika wilaya hiyo.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kufungua kongamano la maendeleo ya Wilaya ya hiyo ambalo lilishirikisha wadau mbalimbali wa kutoka ndani na nje ya wilaya hiyo lilofanyika ukumbi wa chuo cha ufundi Veta Wilayani hapa.
Aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kushirikiana katika kuhakikisha wanafanikisha malengo ya maenedeleo ya kiuchumi yaliyokusudiuwa katika eneo lao.
”Malengo ya kongamano hilo ni kuwaleta pamoja makundi ya wawakilishi wa wananchi kutoka wilaya nzima ili kujadiliana na kupanga maendeleo ya wilaya hiyo”amesema Emanuel
Hivyo kongamano hilo litatoa taswira ya shughuli zilizofanyika na ambazo zinakusudiwa katika kuleta maendeleo ya watu wa Kongwa .
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ,Dk Omari Mkulo alisema kongamano hilo limeshirikisha makundi mbalimbali ya wananchi wa wilaya hiyo.
Dk Mkulo aliyataja makundi hayo kuwa ni wakulima ,wafugaji ,viongozi wa kidini na kisiasa ,wafanyabiashara pamoja na wadu wa maendeleao kutoka ndani na nje .
”Kongamano hilo wameandaa mada mbalimbali zilizotolewa na wataalamu wa ndani ya wilaya na wengine nje ya waialya hiyo”amesema Dkt.Mkulo
Pia alisema wameshirikisha wataalamu kutoka mabenki,shirika la viwangoa Tbs na wataalamu wa sense ambao walitoa elimu kuhusu zoezi la sense ya makazi ya watu inayokusudiwa kufanyika mwakani 2022.
Kwa upande wake Spika wa Bunge ,Job Ndugai aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kushirikiana katika kukuza elimu ambayo ndio msingi wa maendeleo
”Suala la elimu linamhusu kila mwananchi wa wilaya hiyo pamoja hivyo kila upande uhakikishe unasimamia sekta ya elimu kwa kusaidia ujenzi wa madarasa na ununuzi wa madawati kwenye shule zilizopo kwenye maneno yao”amesema Mhe Ndugai