Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Ramadhan Kapela (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda(kushoto) na Katikati ni Mkurugenzi Mteandaji wa Manispaa ya Tabora Dkt.Peter Nyanja
Mkuruenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Dkt. Peter Nyanja akizungumza na waandishi wa habari leo.
Picha na Tiganya Vincent
****************************
NA TIGANYA VINCENT
HALMASHAURI ya Manispaa ya Tabora imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 884 ambayo ni sawa na asilimia 18 ya makadirio ya kukusanya bilioni 4.6.
Takwimu hizo zimetolewa leo na Mkurugenzi |Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Dkt. Peter Nyanja wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Alisema makusanyo hayo ni miezi miwili ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha unaoendelea.
Dkt.Nyanja alisema lengo lao ni kuhakikisha kabla ya kumalizika kwa robo ya kwanza wawe wamekusanya asilimia 25 ya makisio na kufikia bilioni 1.1.
Alisema mafanikio hayo yameanza kuonekana baada ya kubadilisha Watumishi waliokuwa wakihusika na ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuongeza nguvu ya ukusanyaji kwa kubuni vyanzo vipya.
Dkt.Nyanja aliongeza kuwa mwishoni mwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha huu wanatarajia kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ya kiasi cha milioni 100.
Aidha Dkt.Nyanja amevitaka vikundi vinavyokopeshwa fedha kuhakikisha vinazitumika katika kuimarisha mitaji yao ili wawaachie fursa watu wengine kunufaika na mikopo.