************************
Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imerudi usiku wa kuamkia leo ambapo timu kadhaa zimeingia uwanjani kusaka alama tatu ili kuwezesha kuongoza kundi na kuweza kufuzu hatua inayofuata.
Katika michezo ambayo imepigwa usiku huu tumeshuhudia Machester United kupokea kichapo cha mabao 2-1kutoka kwa Young Boys kwenye mchezo ambao ulipigwa mapema majira ya ya saa moja jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Manchester United walianza kupata bao dakika 13 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wao Christiano Ronaldo bao ambalo lilidumu mpaka kipindi cha pili.
Dakika 35 ya mchezo Wan Bissaka beki wa pembeni wa Manchester United alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Young Boys na kuwafanya kucheza pungufu.
Kipindi cha pili Young Boys walitawala mchezo na kuweza kusawazisha bao dakika ya 66 kupitia kwa nyota wao Ngamaleu na baadae dakika ya 94 Theoson kupachika bao la pili na kuwafanya waondoke na uahindi wa mabao 2-1.
Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Chelsea Fc dhidi ya Zenit St.Petersburg ambapo Chelsea iliibuka na ushindi wa bao 1-0 bao ambalo lilifungwa na mshambuliaji wao Romelu Lukaku dakika ya 69 ya mchezo.
Bayan Munich waendeleza ubabe kwa timu ya Barcelona baada ya kuwachakaza kwa mabao 3-0.
Mabao yalifungwa na Thomas Mueller dakika ya 35 ya mchezo na baadae Robert Lewandowsk kufunga bao la pili dakika 56 kilindi cha pili na kufunga bao la tatu dakika ya 85.