Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akikagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma (Dodoma Institute of Technology) kinachojengwa katika eneo la Nala jijini Dodoma leo September 13,2021
Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga,akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma (Dodoma Institute of Technology) kinachojengwa katika eneo la Nala jijini Dodoma leo September 13,2021
Naibu Waziri Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akikagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mfano inayojengwa Iyumbu jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mfano Iyumbu jijini Dodoma leo
Muonekano wa hatua za Mabweni ya Wavulana katika Shule ya Sekondari ya Mfano inayojengwa katika eneo la Iyumbu jijini Dodoma.
***************************
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe Omary Kipanga ametembea na kukagua maendeleo ujenzi wa Chuo cha Ufundi Dodoma(Dodoma Institute of Teknology) kinachojengwa eneo la Nala Jijini Dodoma kinachoghalimu zaidi ya bilioni 17.9 katika ujenzi wake ambapo kitakapo kamilika kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi zaidi ya elfu tatu (3000).
Akizungumza leo September 13,2021 mara baada ya kukagua ujenzi huo Naibu Waziri Kipanga amesema lengo la kujenga chuo hicho ni kuzalisha vijana wengi wenye ujuzi ambao watakwenda kutumika katika viwanda mbalimbali vinavyoendelea kujengwa.
“Ujenzi umeanza mwezi june na unatarajiwa kumalizika mwezi Desemba 2022 na ujenzi unaendela vizuri unajua nchi inakwenda katika viwanda hivyo tumepanga kuzalisha wataalamu wengi katika vyuo hivi” amesema Kipanga.
Amesema lengo la Chuo hicho ni kuwezesha vijana wengi kupata ujuzi, kuzalisha vijana wenye ujuzi wa kati, Serikali imejipanga kujenga Vyuo vya Ufundi katika kanda zote
ikiwemo kanda ya Kati, kanda ya ziwa, kanda ya Kusini na kanda ya kaskazini.
Kwa upande kwake, Mhandisi Msaidizi kutoka Kampuni ya BICO, Aliki Nziku amesema mradi huo mpango wa Serikali kuongeza Wataalam katika nyanja za ufundi na Teknolojia maabara.
Amesema mradi huo unajengwa na Mkandarasi CRJE limited kwa gharama ya Sh bilioni 17.9 chini ya usimamizi wa washauri waandamizi wa BICO na watahakikisha kinakamilika kwa wakati ndani ya miezi 18.
Pia Naibu Waziri Kipanga ametembelea ujenzi wa shule ya Sekondari mfano iliyopo Iyumbu Jijini Dodoma inayojenga na SUMA JKT kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 17 ambayo inatarajiwa kuanza kuchukua wanafunzi mwezi January 2022.
Kipanga amesema wanatarajia kujenga Shule kwa kila Kata nchini lengo ni kuhakikisha kila halmashauri inakuwa na shule za seondari ambazo itasaidia wanafunzi kutotembea kwa umbali mrefu.
“Serikali inatarajia kuanza zoezi hilo mara mikakati walioipanga
itakapokamilika,wanahitaji kuona wanafunzi wanasoma kwa raha kila mahali,”amesema Kipanga.
Naibu Waziri Kipanga wataka Shirika la Ujenzi Suma JKT kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa Shule ya sekondari ya Mfano ya Iyumbu Desemba mwaka huu ili mwakani wanafunzi waanze kusoma.
Amesema awali Shule hiyo ilipangwa kukamilika Februari 2022 lakini ameagiza Shule hiyo ikamilike Desemba Ili ifikapo Januari mwakani ianze kuchukua wanafunzi wa Sekondari.
“Naagiza ujenzi ikamilike Desemba ili Januari wanafunzi wadahiliwe kwa ajili ya kuanza masomo,” amesema Kipanga.
Akitoa taarifa ya Ujenzi kwa Naibu Waziri, Naibu Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Suma Meja Geoffrey Ngole amesema ujenzi ulianza Julai 2020 na utakamilika Februari mwaka 2022 lakini kwa ombi la serikali mradi utakamilika Desemba na sasa ujenzi upo asilimia 60.
“Tumepokea maagizo ya Naibu Waziri ya kukamilika Kazi ifikapo Desemba, tutaongeza nguvu Kazi na tutafanya Kazi usiku na mchana Ili tumalize kwa muda uliotajwa na Naibu Waziri,” amesema Meja Ngole