************************************
Timu ya Mwanza Queens inatarajia kuchuana na Timu ya Jonas Queens katika mashindano ya Angeline Jimbo Cup hatua ya fainali siku ya Ijumaa baada ya kufuzu Kwa kuichapa vikali Timu ya Green Star magoli matano Kwa sifuri.
Akizungumza mara baada ya kuisha kwa mchezo huo, Nahodha wa timu hiyo Aisha Juma amesema kuwa timu yake ina uzoefu wa kutosha na mashindano ya aina hiyo na ilijiandaa vizuri hivyo matokeo walioyapata ni zao la jitihada walizozifanya kabla ya mchezo huo
‘.. Tunashukuru Kwa matokeo mazuri tuliyoyapata na tunaamini tutaibuka mabingwa wa mashindano haya Kwa upande wa wanawake Kwa sababu hata Leo tumeshinda Kwa kujituma na kujiandaa ..’ Alisema
Aidha Nahodha huyo amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula Kwa kuanzisha mashindano hayo na kuamua kuzihusisha timu za wanawake pamoja na kuomba kuendelezwa Kwa utaratibu huo
Nae mchezaji wa timu ya Jonas Queens Marry Peter amesema kuwa mchezo wao dhidi ya TSC Academy ulikuwa mgumu kiasi Cha kushindwa kufungana katika kipindi Cha dakika tisini badala yake kufanikiwa kufuzu Kwa hatua ya mikwaju ya penati baada ya kushinda penati nne Kwa mbili hivyo kuwaomba Mashabiki wa Timu Yao kujitokeza Kwa wingi siku ya fainali kuishuhudia timu Yao pendwa ikiibuka kidedea
Akihitimisha Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Kwa Wanawake Mkoa wa Mwanza (TWFA) Sophia Makilagi amempongeza muasisi wa mashindano ya Angeline Jimbo Cup ambae pia ndie Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula Kwa kubuni mashindano hayo na Kwa mwaka huu kuamua kushirikisha timu za wanawake huku akiomba wadau wengine kujitokeza na kuunga mkono timu za wanawake zinazopatikana ndani ya mkoa huo
Fainali za mashindano ya Angeline Jimbo Cup 2021 Kwa timu zote za wanaume kutoka katika kata na zile za timu ya wanawake zitafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba siku ya Ijumaa ya Septemba 17, 2021 kuanzia saa4 asubuhi.