Bwana harusi Victor Christopher akiwa na mkewe Cherly Mwaka baada ya kufunga ndoa yao katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Uharika wa Mtinko uliopo Wilaya ya Singida Vijijini mkoani Singida jana na kufuatiwa na sherehe iliyofanyika Ukumbi wa.Darabe uliopo eneo hilo la Mtinko.
Maharusi Victor Christopher na mkewe Cherly Mwaka (katikati) wakiwa na wapambe wao Elinuru Elisha na Anna Richard baada ya baada ya kufunga ndoa.
Bwana harusi Victor Christopher akiwasalimia wageni waalikwa waliofika kwenye sherehe ya ndoa yao
Baba na Mama wa Bwana harusi Mzee Christopher Philip Majii na Mke wake Josephine Mohamed Majii wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wazazi wa Bibi harusi wakiwasalimia wageni waalikwa waliofika kwenye sherehe hiyo.
Ibada ya ndoa takatifu ikiendelea katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mtinko.
Bibi na Babu wa Bwana harusi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanakwaya ya Kalvary wakitoa burudani kwenye sherehe ya ndoa hiyo.
Maharusi wakivikana pete.
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mtinko, John Kibuga akitoa baraka kwa maharusi baada ya kufungisha ndoa hiyo.
Bwana harusi Victor Christopher akisaini shahada ya ndoa kabla ya kukabidhiwa.
Kaka wa Bwana harusi Charles Christopher akizungumza kwenye sherehe hiyo.
Maharusi wakionesha shahada za ndoa baada ya kukabidhiwa.
Wanakamati ndogo ya sherehe hiyo kutoka Singida mjini wakifanya yao jukwaani kwenye sherehe hiyo.
Sherehe ikiendelea.
Maharusi wakikata keki.
Dada wa Bwana harusi Christina Christopher (kulia) akiahidi kutoa kabati lenye thamani ya Sh.350,000 kwa mdogo wake ikiwa ni zawadi yake baada ya kuoa.
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ndogo ya sherehe hiyo kutoka Singida mjini, Judith Ngussa akizungumza kwenye sherehe hiyo.
Maharusi wakiwa na wajumbe wa kamati zote za sherehe hiyo.
Baba na Mama wa Bwana harusi Mzee Christopher Philip Majii na Mke wake, Josephine Mohamed Majii wakiwa wamejifunika kwa moja ya zawadi ya vitenge waliokabidhiwa kwenye hafla hiyo.
Wajumbe wa kamati ndogo ya sherehe hiyo kutoka Singida mjini wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Picha ya pamoja na maharusi.