Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari leo September 12,2021 jijini Dodoma kuhusu uzinduzi wa Kitabu cha Mkakati wa uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 utakaozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan September 14,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu,Daniel Masolwa,akieleza jambo kwa waandishi wa habari leo September 12,2021 jijini Dodoma kuhusu uzinduzi wa Kitabu cha Mkakati wa uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 utakaozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan September 14,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
……………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan anatarajiwa Kuzindua Kitabu cha Mkakati wa uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 jijini Dodoma.
Hayo yamesemwa leo,Septemba 12,2021 jijini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka wakati akizunguza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa tukio hilo ambapo amesema linalenga kuandaa umma na wadau kwa ujumla kwa ujio wa sensa ya watu na makazi ya mwaka ujao.
Amesema uzinduzi huo unaokwenda na kauli mbiu inayosema sensa kwa maendeleo,jiandae kuhesabiwa,utafanyika Septemba 14 uwanja wa Jamhuri jijini hapa kuanzia saa 1 asubuh na utahudhuriwa na Vingiozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa kamati ya Kuu ya sensa,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Kassim Majaliwa na Mwenyekiti mwenza kutoka Zanzibar,Makamu wa pili wa Rais Hemed Suleiman Abdallah.
Amewataja viongozi wengine kuwa ni Kamisaa wa sensa Tanzania Bara ,Anne Makinda,Kamisaa wa sensa Zanzibar ,Balozi Mohamed Haji Hamza ,pamoja na Mawaziri,Manaibu Waziri ,Makatibu wakuu ,Manaibu katibu wakuu na viongozi wa serikali kutoka Mikoa minne.
“Viongozi wa serikali kutoka Mikoa minne watashiriki,Mkoa wa Singida,Iringa, Morogoro na Manyara hivyo hata wananchi wa wadodoma wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono Rais wetu kwasababu sensa ni jambo letu wote,”amesema Mtaka
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu,Daniel Masolwa amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu ndio inajukumu la kuratibu masuala ya sensa hivyo tayari imeshaandaa sensa ya majaribio ambayo tayari inafanyika Katika Mikoa 13.
Amesema lengo la sensa ya majaribio kuwa ni kupima na kuhakiki vitendea kazi na Kama vitakuwa na changamoto virekebishwe.