Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai,akiwasili katika eneo la Nane Nane kwa ajili ya uzinduzi wa Muungano wa wadau wa kupambana na kifua kikuu Tanzania ulioshirikisha wabunnge, viongozi wa Dini na Taasisi zingine hafla hiyo imefanyika leo September 11,2021 jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai,akiteta jambo na Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel wakati wa uzinduzi wa Muungano wa wadau wa kupambana na kifua kikuu Tanzania ulioshirikisha wabunnge, viongozi wa Dini na Taasisi zingine hafla hiyo imefanyika leo September 11,2021 jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Muungano wa wadau wa kupambana na kifua kikuu Tanzania ulioshirikisha wabunnge, viongozi wa Dini na Taasisi zingine hafla hiyo imefanyika leo September 11,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Muungano wa wadau wa kupambana na kifua kikuu Tanzania ulioshirikisha wabunnge, viongozi wa Dini na Taasisi zingine hafla hiyo imefanyika leo September 11,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI, Mhe. Fatma Taufiq,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Muungano wa wadau wa kupambana na kifua kikuu Tanzania ulioshirikisha wabunnge, viongozi wa Dini na Taasisi zingine hafla hiyo imefanyika leo September 11,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Muungano wa wadau wa kupambana na kifua kikuu Tanzania ulioshirikisha wabunnge, viongozi wa Dini na Taasisi zingine hafla hiyo imefanyika leo September 11,2021 jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai,akizindua Muungano wa wadau wa kupambana na kifua kikuu Tanzania ulioshirikisha wabunnge, viongozi wa Dini na Taasisi zingine hafla hiyo imefanyika leo September 11,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Watu 74 hufariki kila siku kwa kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) nchini Tanzania huku idadi ya wagonjwa wa kifua kikuu sugu ikiwa juu.
Kwa idadi hiyo, ni sawa na idadi ya abiria wanaosafiri katika basi lenye uwezo wa kubeba watu 65 hadi 70 ambao wangeweza kukaa katika siti na wengine kusimama kutokana na kujaza kupita uwezo.
Takwimu hizo ni za mwaka 2018 ambazo zilitolewa leo September 11,2021 jijini Dodoma na serikali wakati wa uzinduzi wa Muungano wa wadau wa kupambana na kifua kikuu Tanzania ulioshirikisha wabunnge, viongozi wa dini taasisi zingine.
Akitoa taarifa kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali wabunge vinara wa kupambana na TB, Dk Saitole Laizer amesema ugonjwa huo bado ni tishio nchini ingawa watu wengi hawajui kuwa unaua na utaendelea kuua ikiwa juhudi za makusudi hazitachukuliwa kwa haraka.
Dk Saitole amesema kuwa vipimo vinaonyesha kati ya watu 133,000 wanaofikiwa kwa ajili ya vipimo vya TB, 227 hukutwa na maambukizi ya ugonjwa huo ambao kwa sasa Tanzania ina jumla ya wagonjwa wenye TB sugu 1600 nchini kote, 400 wakigundulika mwaka jana pekee.
Hata hivyo Dk Laizer ametaja changamoto ni kutokuwafikia baadhi ya makundi yenye uhatarishi wa ugonjwa ikiwemo watumiaji wa dawa za kulevya na wanaojidunga sindano aliosema ni miongoni mwa makundi hatari zaidi.
“Serikali imetupatia fedha nyingi ambazo zimefanikisha kununua magari mapya matano yatakayofanya kazi hadi vijijini kwa ajili ya vipimo vya kwa watu wanaoshindwa kufika hospitalini, hivyo mapambana haya yanatakiwa kuwa endelevu kwa nguvu na kwa kila mmoja wetu,” amesema Dk Laizer.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel amesema kuwa Wizara imepokea Sh97 bilioni kutoka Serikalini ambazo zinakwenda kupambana na maambukizi ya TB ikiwemo kuimarisha huduma za afya vijijini na kupata takwimu sahihi.
”Wanatarajia kuwafikia watu wengi kwa kutumia magari ambayo Mobile kliniki jambo alilosema linakwenda kumaliza changamoto ya ugonjwa huo na kupeleka elimu ya moja kwa moja kwa jamii ya chini akisema lengo la kutokomeza TB ifikapo 2030 wanaamini kuwa litafikiwa”amesema Dkt.Mollel
Aidha Dkt.Mollel amezungumzia Muswaada wa Bima ya afya kwa wote sasa umeiva kwani hivi karibuni ulitoka mikononi mwa kamati ya Makatibu Wakuu na sasa unapelekwa baraza la Mawaziri ili waupitie na kuuwasilisha bungeni Novemba mwaka huu.
Dk Mollel amesema Muswada huo ulikwama katika haua moja kwa miaka nane lakini jambo jema umekamilika na umepita hatua hiyo hivyo akaomba wabunge kuusubiri kwani utaingia bungeni Novemba mwaka huu.
Akizindua muungano huo Spika wa bunge Job Ndugai amesema kuwa TB ni miongoni mwa magonjwa yanayoua kwa wingi Tanzania na duniani ambayo hayatakiwi kufanyiwa mchezo katika mapambano yake.
Spika Ndugai amewataka Watanznaia kujihadharisha na kuchukua hatua wanapoona kuna dalili kwani ugonjwa unaweza kumpata mtu yeyote na wakati wowote lakini akaomba taasisi ziwekeze fedha kwa vyombo vya habari ili elimu ya ugonjw ahuo ipelekwe hadi maeneo ya vijijini.