Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Athony Mtaka,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bar ya Kusila na Lounge iliyopo Ipagala Jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo September 11,2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Athony Mtaka,akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Bar ya Kusila na Lounge iliyopo Ipagala Jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo September 11,2021.
Mkurugenzi Mtendaji Bar hiyo,Geofrey Kusila,akielezea jinsi alivyopambana mpaka kufika hatua hiyo wakati wa uzinduzi wa Bar ya Kusila na Lounge iliyopo Ipagala Jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo September 11,2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Athony Mtaka,akimsikiliza Mzee William Kusila akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bar ya Kusila na Lounge iliyopo Ipagala Jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo September 11,2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Athony Mtaka,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Bar ya Kusila na Lounge iliyopo Ipagala Jijini Dodoma hafla iliyofanyika leo September 11,2021.
Muonekano wa Bar ya Kusila na Lounge iliyopo Ipagala Jijini Dodoma iliyozinduliwa leo September 11,2021.
…………………………………………………………………
Na Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Athony Mtaka amewataka wakazi wa Dodoma kuchangamkia fursa ya kuanzisha miradi mbalimbali huku akisisitiza umuhimu wa kuweka huduma nzuri katika bishara hizo.
Kauli hiyo ameitoa leo September 11,2021 wakati wa akizindua Bar ya Kusila na Lounge iliyopo Ipagala Jijini Dodoma,Mtaka amesema anatamani mmiliki wa Bar hiyo ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini Kusila amesema anatamani aende mbele katika biashara hiyo kwa wa hudumu kujali wateja.
“Natamani uende mbele ukiona mtu ametoka mbali amekuja hapa mjali sana huyo mteja, Shida moja ya wahudumu ya watanzania anaanza kupika chai ya maziwa wakiongezeka wateja anaweka maji sasa hili liangalieni,”amesema Mtaka
Aidha,RC Mtaka amemtaka mmiliki wa Bar hiyo kuweka mshindani wake kibiashara ikiwani pamoja na huduma nzuri ambazo zitamfanya mteja arudi tena.
“Unafanya biashara Dodoma bahati nzuri umesoma seti mshindani wako ni nani nataka mtu akija aseme naenda sehemu fulani nani ndio mshindani wako,usipoweka mshindani hii gharama uliyoweka hapa ukazidiwa na mchoma ‘Kitimoto’ ambaye atakuwa anauza kuliko wewe kama unatakaka kuwa mtu wa keshokutwa mtafute mshindani wako.
“Na kesho utengeneze vizuri sio leo hawa wahudumu lazima uwafanyie mentaship shida moja ni hawa wakwetu seriousness ni ndogo maintain standard sisi wateja tupo,lakini soko ni huria lazima kuwe na huduma nzuri, oda mtu akikutumia iheshimu sio akija mteja kwa sababu ni Mkuu wa Mkoa atapata lakini akija mwingine anaita tu.
Mtaka pia amewataka vijana wanaioshi nje ya Nchi kuchangamkia fursa ya kurudi nyumbani na kuchangamkia fursa ya uwekezaji nchini na wasisubiri mpaka wawe wazee.
“Somo kwa vijana ungechelewa kurudi usingefanya hichi wewe ni somo zuri kwa wenzako walioko nje anarudi hapa anakiswahili kireeefu lakini sasa wewe umerudi mapema muwe mnashauriana kwenye magroup.
“Kwahiyo ni somo zuri kwa vijana unaenda unakaa nje zaidi ya miaka 50 ukirudi umezeeka na wale waliokuwa vijana wenzako nao wamezeeka unabaki unashangaa tu unakuja na mradi wa solar kumbe vijiji vyote vina umeme,”amesema.
Pia amewataka wakazi wa Dodoma kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo zipo Jijini humo kwani kwa sasa kuna biashara nyingi za kuanzisha.
“Watu wa Dodoma ni vizuri kushikamana Dodoma kuna fursa nyingi naomba jambo hili lisimamia vizuri hasa kwenye huduma.Kwenye biashara epuka kuhudumia watu fulani wenye classic weka wateja vizuri weka oda zako vizuri wapishi wako tunataka kuona huduma msilete mambo ya kujuana hapa mmewekeza hela kuna migahawa wanaoda maofisini wanapeleka,”amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Bar hiyo,Geofrey Kusila amesema huduma mbalimbali zitapatikana katika Bar hiyo ikiwemo uuzwaji wa nyama ya Nguruwe iliyochomwa.
Amesema wakati anaanza biashara hiyo Jijini Dar es salaam wengi walimbeza lakini kwa sasa anamshukuru mungu kwani inaenda vizuri na wateja ni wengi na ameweza kutoa ajira kwa vijana 20.
“Wakati naanza hii biashara kuna wenzangu walinibeza kidogo na nilianza kwa taabu na nilianza Kg mbili nikawaalika rafiki zangu wakaniunga mkono.Haikuwa rahisi hata mke wangu alinibishia hiyo ilikuwa Dar es salaam wateja walikuwa wachache na baadae ikaingia Covid hali ikawa mbaa zaidi.
“Nikamwambia mpishi wangu hebu twende Makao Makuu Mchomaji akaniambia Dar tumeshindwa huko tutaweza kweli,tumepambana mpaka tumefika hapa namshukuru sana Mungu ni mwema sana nikaomba niwaite niwashirikishe kwenye maisha tusikate tamaa nina vijana zaidi ya 20 nimewaajiri,”amesema.