Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akifungua mafunzo kwa wajasirimali wasindikaji wa korosho wilayani Tandahimba ambapo mafunzo yameandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
******************************
Mafunzo yanayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa Wajasiriamali, Wasindikaji wa Korosho na bidhaa za korosho wilayani Tandahimba mkoani Mtwara ni njia muafaka wa kuleta tija zaidi katika juhudi za kuliletea taifa maendeleo ya haraka kulingana na fursa zilizopo hasa kwenye sekta ya viwanda,kilimo,biashara na maeneo mengine mengi.
Ameyasema hayo leo Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala wakati akifungua mafunzo kwa wajasirimali wasindikaji wa korosho wilayani Tandahimba ambapo mafunzo yameandaliwa na TBS.
Amesema kuna umuhimu mkubwa wa watendaji wa halmashauri kushirikiana na TBS ili kuweza kuwahudumia wananchi katika halmashauri hhiyo kwa ufanisi unaotakiwa hasa katika masuala ya viwango kwenye bidhaa wanazozalisha.
“Niwatake TBS kuendelea kuongeza nguvu katika kuboresha mahusiano haya na halmashauri yetu hasa katika kushirikiana kwa ukaribu na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri”. Amesema Kanali Sawala.
Kwa upande wake Meneja wa Mafunzo na Utafiti wa TBS Bw. Hamis Sudi amesema mafunzo hayo yatawasaidia wazalishaji na wasindikaji wa korosho kuzalisha korosho iliyobora na kukidhi viwango ambyo itamfanya apate soko la uhakika hapa nchini na nje ya nchi.
Amesema watawafikia wazalishaji hao mpaka katika maeneo ambayo huanya shughuli zao ili kuweza kuwaelekeza utaratibu bora unaotakiwa katika uzalishaji kuanzia wanapopokea malighafi mpaka hatua ya mwisho ya ufungishaji kwenye vibebashio.