Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji
(Mst) Mary Longway, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya
wasimamizi wa Uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo na
Kata yanayofanyika Mkoani Morogoro kuanzia leo 10 hadi 12 Septemba,2021.
Baadhi ya washiriki ambao ni wasimamizi wa
uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata
wakifuatilia mafunzo ya usamizi wa uchaguzi yaliyoanza leo Septemba 10 na
kumalizika Septemba 12,2021 mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Uchaguzi,Emanuel Kawishe,akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume.
akizungumza wakati wa kuwaapisha Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wa
Saidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata wakati wa kuanza mafunzo yao mkoani
Morogoro.
wasaidizi wa Uchaguzi wakila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi ,Maua Rashid Hamduni ambapo walikula kiapo cha kutunza siri na kujiondoa kuwa wanachama wa vyama vya siasa.
Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wakisaini hati za kiapo baada ya kula viapo vya kutunza siri na kujiondoa kuwa wanachama wa vyama vya siasa.
Na Mwandishi Maalum, Morogoro
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka
Wasimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la
Ushetu katika Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga na Kata za Tanzania
bara kutokufanya kazi ya Uchaguzi kwa mazoea na badala yake wazingatie
maelekezo, kanuni na sharia za uchaguzi katika utendaji wao.
Tume pia imewataka wasimamizi hao na
wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kuhakikisha wanavishirikisha Vyama vyote
vya Siasa na Wadau wengine ili kurahisha
utekelezaji wa majukumu yao.
Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), Jaji (Mst) Mary Longway wakati akifungua mafunzo ya siku tatu
ya wasimamizi wa Uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo na
Kata yanayofanyika Mkoani Morogoro.
“Nachukua nafasi hii kuwaasa kuwa pamoja na
uzoefu ambao baadhi yenu mnao katika uendeshaji wa uchaguzi, ni vyema mhakikishe mnazingatia
maelekezo mtakayopewa na Tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea”,alisema Jaji
(Mst) Longway.
Aidha amewataka kujiamini na kufanya kazi kwa
weledi, na kwamba katika utendaji wa majukumu yao wanapaswa kuzingatia Katiba
ya Nchi, Sheria za Uchaguzi na Kanuni zake, Maadili ya Uchaguzi na Maelekezo
mbalimbali yanayotolewa na Tume na kuongeza kua jambo hilo lisiishie katika
mafunzo na nadharia bali ionekane kufuatiwa katika kutenda.
“Sanjari na hilo nawaasa kukumbuka
kuvishirikisha Vyama vya Siasa na wadau wengine wa uchaguzi katika maeneo yenu katika masuala ya kiuchaguzi
ambayo wanastahili kushirikishwa kwani jambo hilo litawarahisishia sana utekelezaji wa majukumu yenu,”alisema Jaji
(Mst) Longway.
Wasimamizi hao wametakiwa kuhakikisha
wanayatambua na kuyajua vizuri maeneo
ambayo chaguzi utaendeshwa ikiwemo hali ya miundombinu ya kufika katika Kata na
hasa Vituo vya kupigia kura.
“Mfanye utambuzi wa vituo vya kupigia kura
mapema ili kubaini mahitaji maalum ya vituo husika kwa lengo la kuhakikisha mpangilio mzuri ambao utaruhusu
uchaguzi kufanyika kwa utulivu na amani,”alisema Jaji (Mst) Longway.
Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji
(Mst) Mary Longway pia amewataka wasimamizi hao kuhakikisha kuwa wanaajiri
watendaji wa vituo wenye weledi, wanaojitambua na kwa kadri inavyowezekana
kuacha na undugu au upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya
shughuli za uchaguzi.
Jaji (Mst) Lougway, alisema uchaguzi ni
mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa na
kuzingatiwa kwani hatua na taratibu hizo ndio msingi wa uchaguzi kuwa mzuri
,wenye ufanisi na hivyo utasaidia kuondoa malalamiko au vurugu wakati wa
uchaguzi.
Alisema jambo muhimu wanalotakiwa kuzingatia
Wasimamizi hao wa uchaguzi ni kujiamini na kufanya kazi kwa weredi na
kuzingatia Katiba ya nchi,sheria za uchaguzi na kanuni zake,maadili ya uchaguzi
pamoja na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume.
Aidha Mjumbe wa Tume hiyo ya
uchaguzi,aliwasisitizia wasimamizi hao wa uchaguzi kuhakikisha wanafanya
utambuzi wa vituo vya uchaguzi mapema kwa lengo la kuhakikisha mpangilio mzuri
ambao utaruhusu uchaguzi kufanyika kwa utulivu na amani.
Hata hivyo Jaji huyo Mstaafu alionya
wasimamizi hao wa uchaguzi kuachana na udugu na upendeleo kwa ndugu na jamaa
ambao hawana sifa za kufanya shughuli za uchaguzi na badala yake wawajiri
watendaji wa vituo wenye weredi na wanaojitambua kadri inavyowezekana.
Hata hivyo Mjumbe wa NEC aliwakumbusha
wasimamizi wa uchaguzi kuzingatia kanuni zilizotolewa na Wizara ya Afya,Jinsia
na Watoto juu ya kujikinga na UVIKO 19 wakati wa kipindi chote cha uchaguzi.
“Kama mnavyotambua tupo katika wimbi la
maambukizi ya UVIKO 19, kwa kuzingatia kanuni zilizotolewa na Wizara ya Afya ,
Jinsia, Wazee na Watoto juu ya kujikinga na maambukikizi dhidi ya ugonjwa huu,
Tume inaendelea kuwaasa na kusisitiza kuzingatia maelekezo yote yaliyotolewa na
wataalamu wa Afya kwa kuendelea kuchukua tahadhari za kutosha ikiwemo; Kunawa
mikono kwa kutumia maji tiririka na sabuni, Kutumia Vitakasa mikono (Sanitazer)
na Kuvaa Barakoa,” alisema Jaji (Mst) Longway.
Naye
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Uchaguzi,Emanuel
Kawishe,akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume, alisema uchaguzi huo
mdogo utafanyika katika Jimbo la Konde (Zanzibar) na Jimbo la Ushetu (Shinyanga)
pamoja na kata 10 za udiwani.
Alizitaja Kata hizo na Halmashauri zake
katika mabano ni Kileo (Mwanga DC), Neruma(Bunda)Kagera–Nkanda(Kasulu DC)
Luduga(Wanging’ombe), Vumilia (Urambo),Lyowa (Kalambo),Buyuni(Ilala),
Dongo(Kiteto, )Lighwa(Ikungi) na Ndembezi (Shinyanga).
Mapema kabla ya ufunguzi wa Mafunzo hayo
wasimamizi hao walikula kiapo cha kutunza siri na kiapo cha kujiondoa uanachama
wa vyama vyao vya siasa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Maua Rashid Hamduni