Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akifafanua jambo wakati wa zoezi la uhakiki wa namna vyama vya siasa vinavyotekeleza Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi pamoja na kanuni zake katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) zilizopo Mtaa wa Ufipa Kindondoni jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara, Benson Kigaira na Katibu wa Sekretarieti ya chama hicho Julius Mwita.
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza na Mkaguzi wa Ndani wa Hesabu took Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Peter Lyimo wakifuatilia maelekezo kuhusu rejesta ya mali za chama kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Rodrick Lutembeka (aliyesimama) wakati wa zoezi la uhakiki wa namna vyama vya siasa vinavyotekeleza Sheria zinazosimamiwa na ORPP katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu akizungumza jambo wakati wa zoezi la uhakiki wa namna vyama vya siasa vinavyotekeleza Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi pamoja na kanuni zake katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) zilizopo Mtaa wa Ufipa Kindondoni jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu akionyesha moja ya kurasi ya Sera za chama chao wakati wa zoezi la uhakiki wa namna vyama vya siasa vinavyotekeleza Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi pamoja na kanuni zake jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Ukaguzi wa Ndani toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Mussa Boma aliyekaa akifanya ukaguzi wa nyaraka za fedha za Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA wakati za zoezi la uhakiki wa namna vyama vya siasa vinavyotekeleza sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili leo jijini Dar es Salaam. Waliosimama ni Watumishi wa Idara ya Fedha wa CHADEMA Lucas Mrema(kulia) na John Ngauro. (Picha na: ORPP)