TIMU ya Biashara United imeanza vyema Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya raudi ya awli kwa kuwachapa wenyeji FC Dikhil bao 1-0 mchezo uliopigwa katika
Uwanja wa El Hadj Hassan Gouled Jijini Ville de Djibouti nchini Djibouti.
Bao pekee la Biashara United katika mchezo huo limefungwa na beki Denis Nkane dakika ya 52 na sasa timu hizo zitarudiana Septemba 18 Dar es Salaam.
Mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Hay Alwady Nyala ya Sudan na Al Ahli Tirpoli ya Libya.
Mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Hay Alwady Nyala ya Sudan na Al Ahli Tirpoli ya Libya.