Na Mwamvua Mwinyi ,Pwani
MKOA wa Pwani umejipanga kuongeza mapato ya ukusanyaji mapato kupitia vyanzo vya mapato ya ndani ya halmashauri zake kwa asilimia 100 ili halmashauri hizo ziweze kujitegemea na kutoa huduma za kimaendeleo kwa wananchi .
Pia imeelezwa ,uboreshaji wa utoaji huduma za kijamii utasaidia kuondoa migogoro na matatizo kwa wananchi .
Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Katibu Tawala (RAS) mkoa wa Pwani ,Mhandisi Mwanasha Tumbo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mafunzo ya utawala bora wa fedha unaosimamiwa na shirika la maendeleo la ujerumani GIZ pamoja na kufadhiliwa wadau wa maendeleo wa serikali ya Ujerumani, serikali ya Uswisi kupitia shirika la maendeleo la Uswisi na umoja wa Ulaya.
Tumbo alieleza Kwasasa wapo katika asilimia 80,licha ya halmashauri ya Chalinze kufikia zaidi ya asilimia 100 hivyo watajitahidi halmashauri nyingine zifikie lengo lao.
Nae Raymond Nzali ambaye ni mtaalamu mshauri wa mradi wa utawala bora wa fedha, kutoka GIZ alisema lengo la mafunzo hayo ni kutengeneza mpango kazi kwa ajili ya ukusanyaji wa mapato .
“Tumelenga zaidi kwenye ushuru wa huduma ambapo bado uko chini sana licha ya Halmashauri zilizochaguliwa kuonekana zinafanya vizuri kwenye ukusanyaji”.
Ofisa msimamizi mkuu wa mradi huo toka TAMISEMI, Ismail Chami alisema, wameuingiza mkoa wa Pwani kwenye mradi huo kwani nao una vyanzo vingi vya mapato vipya kupitia viwanda.