……………………………………………………………..
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri, amewataka wakandarasi wanaosimamia mradi wa ujenzi wa barabara za mji wa kiserikali mtumba kuweza kukamilika kwa haraka ifikapo mwezi Desemba mwaka huu.
Agizo hilo amelitoa wakati wa ziara ya kukagua Barabara za TAURA katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ,amesema serikali ilitenga zaidi ya shilingi bilioni 86.3 kwaajili ya kukamilisha mradi huo ambao utatengeneza barabara zote zinazopita katika mji huo wa kiserikali mtumba kwa kiwango cha rami.
Amesema kwa sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 83 hivyo wakandarasi hao watumie uzalendo wao katika kufanikisha barabara hizo zinajengwa kwa ustadi wa hali ya juu, pia aliwataka waweke maboresho kupitia taa za barabarani kuweza kufunga kamera maalumu zitakazo saidia shughuli nzima za ulinzi na usalama kwenye eneo hilo.
“Tunaona TARURA wanajitahidi sana kwenywe ukamilisho wa mradi huu, lakin nacho waomba wafanye kazi kizalendo na kwa kuongezea tu ili mji huu uwe salama zaidi waweze kufunga kamera za kiusalama ata kama kutakuwa na askali” amesema Dc Shekimweri
Kwa upande wake Meneja wa TARURA,Mhandisi Mohamed Mkwata, amesema usanifu wa barabara hizo ni za aina mbili ambao ni njia mbili na njia nne, njia mbili zitakua za umbali wa kilometa 28.8 na njia nne km 11.3, pia alisema barabara hizo zitakuwa sambamba na ujenzi wa madaraja, njia za maji, umeme, gesi pamoja na uboreshaji wa njia za watembea kwa miguu.
Aidha ametaja idadi ya barabara mpaka hivi sasa zimekwisha kamilika ambazo ni zenye urefu wa kilometa 43 zenye kiwango cha rami na kubakiza km 8 ambazo zinaendelea na ukarabati.
Pia amesisitiza pia kuwa mkandarasi aliepewa ujenzi huo ambae ni kampuni ya Chiko kutoka china ana weredi mzuri katika ufanisi kwani mpka hivi sasa serikali imeendelea kumuamini kutokana na kazi yake.
” Ujenzi wa mradi huu ulitakiwa ukamilike mwezi julay mwaka huu lakini kutokana na changamoto zilizozo nje ya uwezo kampuni hii ya chiko imeongezewa muda mpk disemba mwaka huu mradi ukamamilike kwa ustawi wa hali ya juu” amesema Mhandisi Mkwata,