Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Zainabu Chaula akiwa pamoja Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt.Tito Mwanuka wakisaini mkataba wa Mashirikiano kati ya Wizara na taasisi hiyo kwenye ujenzi wa miundombinu ya mkongo kwa kutumia miundombinu ya Umeme, tarehe 7 Septemba,2021. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Zainabu Chaula akibadilishana mikataba na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt.Tito Mwanuka wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la Mashirikiano kwenye ujenzi wa miundombinu ya mkongo kwa kutumia miundombinu ya Umeme, tarehe 7 Septemba,2021.Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la Mashirikiano kwenye ujenzi wa miundombinu ya mkongo kwa kutumia miundombinu ya Umeme, tarehe 7 Septemba,2021. Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la Mashirikiano kwenye ujenzi wa miundombinu ya mkongo kwa kutumia miundombinu ya Umeme, tarehe 7 Septemba,2021.Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Zainabu Chaula akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la Mashirikiano kwenye ujenzi wa miundombinu ya mkongo kwa kutumia miundombinu ya Umeme, tarehe 7 Septemba,2021.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe.Seleman Kakoso akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la Mashirikiano kwenye ujenzi wa miundombinu ya mkongo kwa kutumia miundombinu ya Umeme, tarehe 7 Septemba,2021. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la Mashirikiano kwenye ujenzi wa miundombinu ya mkongo kwa kutumia miundombinu ya Umeme, tarehe 7 Septemba,2021.Mtendaji Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw.Waziri Kindamba akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la Mashirikiano kwenye ujenzi wa miundombinu ya mkongo kwa kutumia miundombinu ya Umeme, tarehe 7 Septemba,2021.
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt.Tito Mwanuka akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la Mashirikiano kwenye ujenzi wa miundombinu ya mkongo kwa kutumia miundombinu ya Umeme, tarehe 7 Septemba,2021. Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.Faustine Ndugulile (kushoto aliyekaa) na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia aliyekaa) wakipata picha ya pamoja na viongozi wa taasisi mbalimbali. Waliosimama kuanzia kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi,Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt.Tito Mwanuka,Mtendaji Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw.Waziri Kindamba na Kaimu Posta Masta Mkuu, Macrice Mbodo wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la Mashirikiano kwenye ujenzi wa miundombinu ya mkongo kwa kutumia miundombinu ya Umeme, tarehe 7 Septemba,2021. Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari Dkt.Faustine Ndugulile (kushoto aliyekaa) na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia aliyekaa) wakipata picha ya pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe.Seleman Kakoso (wa pili kulia) wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la Mashirikiano kwenye ujenzi wa miundombinu ya mkongo kwa kutumia miundombinu ya Umeme, tarehe 7 Septemba,2021.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
***************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wameingia mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wa Ushirikiano kwenye Ujenzi wa miundombinu ya mkongo kwa kutumia miundombinu ya umeme ambao utawezesha kuokoa usumbufu na gharama zisizo za lazima.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo leo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari Dkt.Faustine Ndugulile amesema utekelezaji wa mkataba huo utasaidia TANESCO kupitisha miundombinu ya umeme kwa kutumia nguzo zitakazokuwa zimejengwa kwa ajili ya miundombinu ya mkongo wa Taifa.
Amesema nguzo zitajengwa kwa viwango sawa na nguzo za sasa za TANESCO na zitajengwa kwa ushirikiano wa pamoja.
“Malengo ya Serikali ya ujenzi wa miundombinu ya mkongo na usambazaji wa umeme yatafikiwa kwa haraka kupitia uwekezaji na matumizi ya pamoja ya miundombinu hiyo”.Amesema Dkt.Ndugulile.
Kwa upande wake Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema kwasasa TANESCO lina miundombinu mingi na mingine inaendelea kujengwa pamoja na Kilomita 3886 za sasa hivi lakini bado wanajenga njia nyingi za kupeleka umeme ambazo mtandao wa TTCL itazitumia.
Aidha Waziri Kalemani amesema ushirikiano huo utasaidia kupunguza gharama ambazo hazikuwa za lazima pia kusaidia kuimarisha mahusiano kati ya sekta hizo ambayo yatasaidia kuimarisha usiamamizi wa miundombinu na kubadilishana utaalamu pamoja teknolojia.
“Maelekezo yangu kwa timu hizi mbili zikae zianze kubadilishana teknolojia ili kusudi tunakokwenda kuwe na miundombinu iliyobora zaidi kwani tutakuwa na miundombinu ambayo ni endelevu”. Amesema Dkt.Kalemani.
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mhe.Seleman Kakoso amesema TANESCO imefanya kazi kubwa ya kupeleka miundombinu ya nishati katika karibu kila hapa nchini hivyo tunategemea Wizara ya Mawasiliano itatumia hiyo miundombinu kupeleka huduma hiyo.
Amesema kupitia mkataba wa makubaliano huo amewataka watendaji ambao wanahusika kuwajibika ipasavyo ili kuwepo kwa matokeo chanya hasa kwa ushirikiano utakaokuwepo baina ya Wizara ya Mawasiliano pamoja na TANESCO.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt.Tito Mwanuka amesema kupitia makubaliano hayo itawasaidia kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi kuliko kama kila taasisi ikiwa inafanyya shughuli hizi kwa peke yake pia tutapata thamani ya fedha ambayo serikali imeitoa.
Vilevile kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw.Waziri Kindamba amesema tunapaswa kuhakikisha umeme pamoja na huduma za mawasiliano zifike katika maeneo mengi hasa vijijini ili wananchi waweze kupata huduma nyingi kupitia sekta hizo.
“Moja ya faida tutakayoipata ni uwekezaji kwa kutumia gharama ndogo pale tutakapotumia miundombinu ya TANESCO, sina tena gharama kama TTCL au kama Mkongo kwenda kununua nguzo wakati TANESCO wanazo nguzo. Kwahiyo hii peke yake inakwenda kushusha gharama za uwekezaji”. Amesema Bw.Kindamba.