Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Said Ntahondi akifungua kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani jana
………………………………………………………………………….
NA TIGANYA VINCENT
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui limewafukuza kazi watumishi 15 kwa makosa mbalimbali.
Kauli hiyo imetolelewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi kwa niaba ya Madiwani wenzake na wakati wa kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani.
Alisema watumishi hao wamefukuzwa kwa sababu ya na makosa ya utoro kazini na wengine walikutwa na vyeti vya bandia(vyeti feki).
Ntahondi alisema watuhumiwa 28 waliokuwa waliokuwa wanakakabiriwa na tuhuma mbalimbali wamefutiwa makosa yao baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kuwaingiza hatiani.
Alisema Mamlaka ya Nidhamu ya Watumishi wa Halmashauri hiyo imemwondoa Mtendaji wa Kata ya Nsololo na kuwamgiza Mkurugenzi Mteandaji kupeleka Mtendaji mwingine baada ya kubaini aliyekuwepo kushindwa kumudu majukumu yake.
Ntahondi aliongeza wamemsimisha Fundi Sanifu wa Halmashauri hiyo kupitisha uchunguzi baada ya kubainika mapungufu katika ujenzi wa baadhi ya Maabara wilayani humo.
Aidha Mwenyekiti huyo aliwaagiza Wakuu wa Idara wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia vema watumishi wanaowasimamia ile waendelee kutoa huduma bora kwa wananchi.