Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wakiimba wimbo wa Taifa kabla Baraza lao halijaanza jana.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Said Ntahondi akifungua kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani jana
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Kisare Makori akitoa salamu za Serikali akati wa kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani jana.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wakiwa kikao cha robo ya nne ya Baraza lao jana.
Picha na Tiganya Vincent
………………………………………………………………………………………….
NA TIGANYA VINCENT
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui limetoa miezi minne kwa kwa Watendaji wanaohusika na ukusanyaji mapato kuhakikisha wamefisha asilimia 100 ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ifikapo Desemba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolelewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi kwa niaba ya Madiwani wenzake na wakati wa kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani.
Alisema miezi ya kukusanya mapato kupitia vyanzo vya ndani imebaki mine ni vema watendaji wakahakikisha wanashirikiana na Madiwani ili watumie miezi iliyobaki kufikia malengo waliyojiwekea ya kukusanya shilingi bilioni 2.4.
Ntahondi alisema Desemba shughuli za kilimo zikianza kama watakuwa hawajaifikia lengo itakuwa vigumu kukusanya kiasi walichojipangia.
Aliwataka Madiwani kuhakikisha wanawasimamia kwa karibu Watendaji wa vijiji ili waweze kuonyesha mpango wao wa ukusanyaji wa mapato na wautekeleze kwa vitendo.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Kisare Makori alisema wakusanyaji wa mapato wanatakiwa kuwa waadirifu kwa kuhakikisha fedha zote zinakusanywa zinakwenda sehemu husika.
“Ndugu zangu Madiwani hakikishe kila senti ya Serikali inayokusanywa inapelekwa katika shughuli za maendeleo ya wananchi…pia hakikishe mnaziba mapengo ya upotevu wa mapato ya Serikali”alisitiza.
Mwisho
MADIWANI WA UYUI WAMWAGIZA DED KUONDOA WAVAMIZI WA MISTU YA HIFADHI YA HALMASHAURI
NA TIGANYA VINCENT
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauuri wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Hemed Magaro ametakiwa kuendesha oporesheni ya kuwaondoa wavamizi ambao wanaendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika mistu ya hifadhi ya Uyui.
Agizo hilo lilitolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi kwa niaba ya Madiwani wenzake na wakati wa kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani.
Alisema wavamizi hao wameingia katika Mistu ya Halmashauri ya Malongo, Kigwa, Kizengi , Tura na kufanya uharibifu kwa kukata miti ovyo na kuendesha shughuli za kilimo ambazo zinatishia suala la ufuagaji nyuki na uhifadhi endelevu wa mazingira.
Ntahondi alisema opesheni ya kuwaondoa wavamizi ikanza sasa kabla ya kipindi cha masika kuanza kwa kuwa wakishalima mazao mbalimbali itakuwa vigumu kuwaondoa kwa sababu ya kuohofia kuharibu mazao yao.
Wakati huo huo Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Uyui limeomba Seketarieti ya Mkoa wa Tabora kufuatilia utaratibu wa kuigawa Halmashauri hiyo ili kusogeza huduma karibu na wananchi.
Ntahondi alisema walishatoa toa ombi hilo tangu mwaka 2012 na Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Tabora (RCC) kikapitisha lakini utekelezaji wake umekwama.
Alisema Halmashauri hiyo ni kubwa ina Vijiji 156 na inapaswa kuwa na Halmashauri mbili ya Igalula na Uyui ili kuondoa usumbufu kwa wananchi kutafuta huduma.
Ntahondi alisema wakazi wa Loya , Tura na maeneo mengine wamekuwa wakitumia gharama kubwa kufuata huduma makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Uyui ambayo yapo Isikizya.
Aliongeza sanjari ba hili aliiomba Serikali kutaka Serikali kutangaza Tarafa ya Kizengi ambayo Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Benjamin William Mkapa wakati wa uongozi wake alitangaza kuanzishwa kwake , lakini hadi hivi sasa bado hajitangazwa katika Gazeti la Serikali.
Alisema kukosekana kwa Tarafa hiyo kunafanya Afisa Tarafa wa Kigwa kuwa na eneo kubwa la Utawala ambalo linazidi baadhi ya Wilaya hapa nchini na kumfanya kutowafikia wananchi wote kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kutoa huduma kwao.