WAZIRI wa Elimu Sayasi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako,akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Jeshi, Kapteni Mturi wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mfano iliyopo Iyumbu jijini Dodoma leo September 6,2021.
WAZIRI wa Elimu Sayasi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako,akikagua ujenzi wa shule ya Sekondari ya mfano iliyopo eneo la Iyumbu jijini Dodoma,wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea shule ili kuona maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo leo September 6,2021.
WAZIRI wa Elimu Sayasi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako,akitoa maelekezo kwa Kampuni ya ujenzi ya Suma JKT inayojenga shule ya Sekondari ya mfano iliyopo eneo la Iyumbu jijini Dodoma,wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea shule ili kuona Maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo leo September 6,2021.
Vijana wa Suma JKT wakiendelea na ujenzi wa shule ya Sekondari ya mfano iliyopo eneo la Iyumbu jijini Dodoma.
WAZIRI wa Elimu Sayasi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichakoakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kukagua na kujionea Maendeleo ya Ujenzi wa shule ya Sekondari ya Mfano iliyopo eneo la Iyumbu jijini Dodoma,wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea shule ili kuona Maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo leo September 6,2021.
Operesheni Kamanda wa mradi huo kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Luteni Kanali Philemon Komanya,akizungumzia walivyojipanga kumaliza ujenzi wa shule ya Sekondari ya Mfano kabla ya mwezi wa Pili mwakani.
…………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Elimu Sayasi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameitaka Kampuni ya ujenzi ya Suma JKT inayojenga shule ya Sekondari ya mfano ya Iyumbu iliopo eneo la Iyumbu jijini Dodoma, kukamilisha ujenzi wa madarasa kabla ya Februali mwakani kama mkataba unavyoelekeza ili wanafunzi waanze kuitumia.
Agizo hilo amelitoa leo September 6,2021 Jijini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo ,Prof.Ndalichako amesema kuwa ni lazima kampuni ya Suma JKT iwe imekamilisha ujenzi wa madarasa kabla ya Februali mwakani kama mkataba unavyoelekeza ili wanafunzi wa kidato cha kwanza waanze masomo.
“Hii shule ni nzuri sana kwa sababu inakila kitu ikiwemo maabara na sehemu za michezo na vitu vingine ambavyo vinahitajika kuwa katika shule.Shule hii imetumia sh billion 17 kwa ajili ya ujenzi ni shule bora ambayo mwakani inahitajika kuanza kutumika na wanafunzi ambao watachaguliwa kuingia kidato cha kwanza,”amesema Prof. Ndalichako.
Amesema kuna mradi uliokuwa ukifanyiwa kazi kwa muda wa kuimarisha elimu ya sekondari ambapo mradi huo tayari umekwishaanza na fedha zimetolewa kiasi cha US Dolla million 74,ambazo ni sawa na bilioni 170 za kitanzania.
Waziri Ndalichako amesema fedha hizi tayari zimekwishapangiwa matumizi na moja ya matumizi ni kwenda kujenga shule za sekondari kwa ajili ya wasichana ambazo ni za Bweni na kwa kuanzia tutaanza na mikoa 10 na kila shule billion nne,huku akisema katika halmashauri zote ambazo wanachukua katika kata ambazo hazina sekondari serikali inakwenda kujenga shule moja.
Amesema zaidi kutakuwa na shule 184 katika halmashauri ukijumlisha na shule 10 za mfano ambazo zitajengwa katika mikoa 10 itakayojulikana hapo baadae mara baada ya waziri wa TAMISEMI atakapotangaza.
“Ujenzi wa shule za sekondari katika Kata ndani ya halmashauri zitagharimu sh million 600 na wa watoto wa kike zitakuwa zinachukua wanafunzi 1,000 na hizo za bweni zitagharimu sh billion nne kilamoja,” amesema Profesa Ndalichako.
Vilevile amesema hivi sasa wako katika hatua za mwisho za kukamilisha kuhamisha fedha kwenda katika halmashauri zao, ambapo Waziri wa Fedha na Mipango ,Tamisemi na Elimu,Sayansi na Teknolojia wanahakikisha wanatekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha ujenzi wa shule unakamilika.
Katika hatua nyingine,Waziri Ndalichako amewataka wasimamizi wa mitihani kuacha tabia ya udanganyifu ikiwemo kuvujisha mitihani ya taifa ya Darasa la Saba inayoanza kesho na keshokutwa hapa nchini badala yake wafanye kazi hiyo kwa weledi ili kuepuka mkono wa sheria.
Amesema katika miaka miwili iliopita kumekuwa na katabia kaudanganyifu kwa wasimamizi wa mitihai ya taifa katika shule mbalimbalihivyo serikali inatoa onyo kwa wasimamizi wenye tabia hiyo kwa sababu wamejianda kuhakikisha watu hao wanabainika na kuchukuliwa hatua kali.
Pia alifafanua zaidi ya kuwa wasimamizi wote wanapaswa kufuata utaratibu na kanuni za usimamizi, katika mitihani ya taifa.
“Naomba wasimamizi wote mfanye kazi ya usimamizi kwa weledi ili wanafunzi watahiniwa wafanye mitihani sahihi kwa kutumia akili zao na uwezo waliofundishwa darasani,”amesema Profesa Ndalichako.
Hata hivyo, amewataka wanafunzi wa Darasa la Saba kujiamini wanapoingia katia mitihani hiyo ya taifa ili waweze kufanya vizuri na kupata ufaulu mkubwa,kwa sababu serikali hivi sasa imewekeza katika suala la elimu kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake,msimaizi wa ujenzi wa mradi wa shule hiyo Luteni Kanali Philemon Komanya amesema ujenzi wa shule hiyo umefikia asilimia 60, ambapo ameahidi kutekeleza ombi la Waziri Profesa.Ndalichako la kuhakikisha shule hiyo inakamilika kabla ya Februali 2022 ili wanafunzi wanaohitimu waweze kuanza kusoma hapo mwakani.