Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna (wa pili kulia) wakifungua milango kuashiria uzinduzi wa Asasi ya Kiraia ya NMB Foundation kwenye ukumbi wa hoteli ya Kilimanjaro-Hyatt jijini Dar es salaam, Septemba 6, 2021. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makala na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NMB, Dkt. Edwin Mhende.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna (wa pili kulia) wakifurahi baada ya kuzindua Asasi ya Kiraia ya NMB Foundation kwenye ukumbi wa hoteli ya Kilimanjaro-Hyatt jijini Dar es salaam, Septemba 6, 2021. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NMB, Dkt. Edwin Mhende.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Benki ya NMB baada ya kuzindua Asasi ya Kiraia ya NMB Foundation kwenye ukumbi wa hoteli ya Kilimanjaro-Hyatt jijini Dar es salaam, Septemba 6, 2021. Waliokaa kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makala, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Dkt. Edwin Mhende, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameipongeza benki ya NMB kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na taasisi za Serikali katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya.
Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 6, 2021) wakati akizindua Asasi ya Kiraia ya NMB. Uzinduzi huo umefanyika katika Hotel ya Kilimanjaro Hyatt jijini Dar es Salaam.
“Nitoe wito kwa taasisi nyingine za fedha na zisizo za kifedha na hata mtu mmoja mmoja kujenga utaratibu wa kurejesha kile kidogo alichoturuzuku Mwenyezi Mungu kwa jamii.”
Waziri Mkuu amesema Serikali inaunga mkono jitihada hizo ambazo zinalenga kupunguza changamoto katika maeneo ya afya, elimu, kilimo, mazingira na ujasiriamali nchini.
Amesema Serikali inaamini kuwa, kuanzishwa kwa asasi hiyo kutaimarisha utoaji wa huduma za kijamii. “Hiki ni kielelezo tosha kuhusu kujitoa kwa NMB kwa jamii inayotuzunguka.”
Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna alisema asasi hiyo inalenga kusimamia na kufuatilia maendeleo ya jamii katika sekta za elimu, afya, kilimo, mazingira na ujasiriamali.
Alisema mbali na asasi hiyo pia benki hiyo imeanzisha mpango maalumu wa kutoa ufadhili wa masomo ya kidato cha tano na sita pamoja na vyuo vikuu kwa wanafunzi wenye ufaulu wa juu lakini wanatoka katika mazingira magumu. “Kwa mwaka huu tutaanza na wanafunzi 200.”