Na Mwandishiw Wetu,Michuzi Blog
Kampuni
ya Unleashed Afrika imeandaa programu maalum inayoitwa UWEZO Tanzania
2021 kwa ajili ya kuwainua wanawake wajasiliamali Jamii, ikiwa ni
mkakati maalum wa kuwainua katika shughuli zao za ujasiliamali.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi na Mwanzilishi wa
kampuni ya Unleashed Afrika, Bi Khalila Mbowe amesema wao pamoja na
mambo mengine wamejikita katika maendeleo ya vijana ,kukuza ubunifu
,kutafuta mbinu tofauti za kuongeza kazi kwa vijana wameona haja ya
kuandaa mafunzo kwa wajasiliamali hao wanawake.
“Tunafanya kazi
nyingi katika eneo hili hasa kwa kumuwezesha mtoto wa kike, tumejikita
katika kukuza ujasiliamali jamii, ili waweze kutatua matatizo kwenye
jamii zao, kitu ambacho tunafahamu watoto wa kike wajasiliamali
wanachangamoto za kipekee , na tumefanya programu tofauti tofauti kama
Tujenge TZ ,sasa hivi tuna mchakato mwingine unaitwa Nipe Dili.
“Lakini
tumekuja kuona wajasiliamali jamii hasa wajasiliamali wa kike wana
changamoto za kipekee na kama tunataka kuwasaidia kutatua hizo
changamoto inabidi kufikiria kwa upana zaidi ni jinsi gani tunaweza
kutengeneza programu ambazo zimejikita kutatua hizo changamoto, wakati
kwa upande wa pili tunawafundisha jinsi ya kukuza ujasiliamali jamii
zao,”amesema Mbowe.
Ameongeza anaposema rasilimali jamii zao
anamaanisha biashara wanazozifanya kwa namna moja au nyingine
zinanyanyuka na zinaleta manufaa kwa jamii.Programu hiyo imeanza mwaka
huu na kwamba Uwezo Tanzania 2021 wamekuwa na ubia na taasisi ya
Kifaransa iitwayo FollowHer.” Tumekuja pamoja tumeleta Uwezo Tanzania na
huu ni mwaka wa kwanza.”
Ameongeza kwamba walianza kufungua
usajili wa mafunzo hayo kwa watoto wa kike wakaweza kuomba , hivyo
wameanza huo mchakato wa kupokea maaombi Februari mwaka huu na mchakato
wa kutengeneza programu umeanza muda mrefu.”Vitu ambavyo tulikuwa
tunajiuliza ni vitu gani ambavyo tuviweke ,kuwe na programu ya aina gani
,
“Tumetumia mawazo mengi sana, tumetumia tafiti nyingi kuweza
kuja kutengeneza kitu kama Uwezo, hivyo kuanzia Februari,Machi,Aprili
watu walikuwa wanajiandikisha ,na Aprili na Mei tulikuwa na watalaam
walioomba kutembelea biashara zao ili kuchagua hawa wajasiliamali wa
kile ambao wamepatikana, wapo 15, Julai wamepatiwa mafunzo mazito kidogo
katika ujasiliamali jamii.
“Baada ya hapo tukawakutanisha na
wakufunzi kwa wiki nne na kila mtu tumemkutanisha na mkufunzi wake ili
wawasaidie kutumia yale mafunzo waliyoyapata darasani ,kwasababu wakati
mwingine unaweza kuwa darasani ukafurahia yale mafunzo lakini ukifika
kazini haviingiliani ,kwa hiyo ikawa ni muhimu kuwakutanisha na watu
ambao watawezesha yale mafunzo kuyaishi katika biashara zao,”amesema.
Amesema
bada ya hapo wakawa na wiki ya mwisho ya mafunzo ambayo ndio hii ya
sasa ambapo wamewakumbusha waliyojifunza na pia wamepanga michakato na
mipango kazi ya miezi sita ijayo.”Siyo tunamaliza programu halafu
tunaagana, je baada ya miezi sita utakuwa umekuza vipi biashara yako?
“Tunakuunganisha
na nani? Halafu leo tumekuwa na shughuli hii ya kuwakutanisha na wadau
wengine kwenye sekta ya ujasiliamali jamii tanzania, kwanini ili
kuhakikisha hawa wajasiliamali jamii wa kike hawaondoki tu na mafunzo
,bali wanaondoka na ‘Conection’ kama tunavyofahamu kitu
kinachomtofautisha ujasiliamali na kukua kwa kasi na yule anayebaki pale
pale ni ‘conection’ na nani anaweza kukufungulia mlango gani.
“Kukupa
mawaidha gani maana tunasema watu wanaokuzunguka ndio watakaoweza
kukunyanyua ,labda kule walipo kuna watu wengi wanawazunguka lakini
hawana mawazo mapya kwa hiyo tumetaka kuwakutanisha na watu ambao
wanaweza kuwapanua zaidi kiakili,”amesema Mbowe.
Amefafanua ndio
maana wamefanya hivyo na baada ya leo kutakuwa na mchakato wa miezi
mitatu kuanzia Septemba,Oktoba na Novemba na katikati ya Desemba
watakuwa wanawakutanisha na watu wengine ambao wataenda kuwasaidia kule
kwenye biashara ili ili kuziimarisha,
“Kwa yule anayependa
kujiunga na UWEZO, huu ulikuwa mwaka wa kwanza na tunaweza kuja na huko
mbele ya safari tutatoa taarifa kuhusu mipango yetu kwa miaka ijayo ,
kwa sasa kuna michakato inaendelea kwa wale ambao walikuwepo tumewaambia
mwaka huu ulikuwa uthubutu , kuonekana,tulikuwa hatuna wafadhili ,hivyo
tumejitolea kwa nguvu na damu jingi kuhakikisha tunafanya hiki kitu na
sasa kimeonekana ,
“Sasa tunatafuta wadau kama umeguswa gonga
mlango njoo utusaidie ,mwaka huu tumefanya Zanzibar, Kisarawe na Dar es
Salaam na tunataka kufanya mikoa mingi zaidi ambayo iko nje ya Dar es
Salaam, tunataka kupata wasichana wengine zaidi ,”amesema.
Mkurugenzi
na Mwanzilishi wa kampuni ya Unleashed Afrika, Bi Khalila Mbowe
akimkaribisha mdau mwenza kutoka taasisi ya FollowHer,Juliette Vigato
kwa ajili ya kukabidhi vyeti vya ushiriki wa Wajasiliamali Jamii ambao
walikuwa wanahitimisha mafunzo yao ya progaramu maalum ya ujasiliamali
‘UWEZO TANZANIA 2021’ .Hafla hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki jijini
Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wahitimu wa progaramu maalum ya kuwainua Wajasiliamali Jamii ‘UWEZO
TANZANIA 2021′ wakifurahia baada ya kupokea vyeti vyao vya ushiriki na
kuhitimisha mafunzo yao wakiwa na Waandaaji wa Mafunzo hayo.
Mkurugenzi
na Mwanzilishi wa kampuni ya Unleashed Afrika, Bi Khalila Mbowe
akiwapongeza baadhi ya Wafanyakazi wake walioshiriki kufanikisha
programu hiyo ya kuwainua Wajasiliamali Jamii.
Baadhi
ya Wahitimu wa progaramu maalum ya kuwainua Wajasiliamali Jamii ‘UWEZO
TANZANIA 2021′ wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea vyeti
vyao vya ushiriki
Mkurugenzi
na Mwanzilishi wa kampuni ya Unleashed Afrika, Bi Khalila Mbowe
akizungumza mbele ya wahitimu wa progaramu maalum ya kuwainua
Wajasiliamali Jamii ‘UWEZO TANZANIA’ pamoja na Wadau wengine wakati wa
hafla fupi ya kuwakabidhi vyeti wahitimu hao na kuwaaga,hafla hiyo
ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo ikiendelea
Wajasiriamalia
hao ‘uwezo Queens’ wakibadilishana mawazo na baadhi ya wadau katika
suala zima la kupeana uzoefu na ‘connection’ katika uwanja wa
Wajasiliamali Jamii
Wajasiriamalia
hao ‘uwezo Queens’ wakibadilishana mawazo na baadhi ya wadau katika
suala zima la kupeana uzoefu na ‘connection’katika uwanja wa
Wajasiliamali Jamii.